Friday, September 18, 2009

Ushauri wa bure kwa walioa na kuolewa!



Nianze kwa kuongea nanyi wanawake wenzangu. Kimaumbile wanaume wanapenda kuona wanasikilizwa na wake zao na hawakawii ‘kukubadilikia’ unapowakwaza. Pamoja na kwamba nanyi mna sauti ndio, lakini wanaume ni watu wa kuwasoma kwanza na kuwaendea taratibu kuliko kuwapandishia na kuonesha kushindikana nao. Kama kweli unampenda basi muoneshe unamheshimu, hapo utampata!

Wanaume hupenda wanawake wasafi, wakarimu, wacheshi na wasio na kiburi wala ‘nongwa’ zisizokuwa na maana, jitahidi katika hayo ili ukonge moyo wa mpenzi wako na kamwe hatakusaliti.

Lakini huwa nasikitishwa sana na hizi zama za usawa ambazo zinachochea migogoro mingi katika ndoa. Kwa mfano, hivi sasa mwanamke kumtii mumewe kunachukuliwa ni kama utumwa!

Nawahakikishia, kwa ninavyofahamu hisia za wanaume walio wengi, hali hii ikiendelea sidhani kama kutakuja kuwa na mapenzi imara, sana sana mapenzi yatageuka kuwa uwanja wa mapambano na ushindani siku zote.

Nawaomba wanawake, pamoja na elimu mliyonayo na visomo vya hali ya juu, jitahidini kujilazimisha kuwaheshimmu waume zenu kwani kamwe hamtapungukiwa na kitu bali mtajihakikishia mapenzi yenye utulivu na amani siku zote za maisha yenu!

Nikiwageukia wanaume, jamani akina kaka na akina baba, ninyi mnachukua nafasi ya baba yenu Adamu. Baba yetu Adamu alimpenda mke wake kwa dhati hata akashawishika kula tunda alilokatazwa ili mradi asimsononeshe mkewe.

Yawapasa mfahamu kuwa wanawake ni zawadi kwenu, pumziko na tulizo la mioyo yenu. Wanawake ndio raha yenu na amani kubwa ya maisha yenu.
Kosa kubwa mnalofanya wanaume ni kuutumia vibaya “mfumo dume” hasa katika suala nyeti kama mapenzi. Mapenzi si ubabe, mapenzi ni upole na ukarimu. Pamoja na kwamba mmebarikiwa kwa kupewa nafasi ya kuwa ‘kichwa katika nyumba’ lakini linapokuja suala la kurekebisha tofauti zinazojitokeza katika uhusiano wenu, si vyema kutumia njia za kibabe.

Niwaambie kitu, wanawake ni wa ‘hisia’ zaidi na waliobarikiwa upendo wa hali ya juu na ndio maana wakapewa dhamana ya kubeba mtoto tumboni kwa miezi tisa na pia kumnyonyesha na kumlea kwa miaka kadhaa, wewe ungeweza?

Nasema ni watu wa hisia kwa sababu, hivi uliwahi kufikiri ni kwanini wanawake huridhika sana na kujisikia poa kweli wanapopewa zawadi kama ya maua na kadi zenye ujumbe wa mapenzi ukilinganisha na wanaume? Unafikiri ni kwanini wana machozi ya haraka wanapotendwa? Au unafikiri ni kwanini wanapenda kutumiwa meseji za kimah aba ‘love message’ zaidi kuliko kupigiwa simu? Jiulize.

Mimi nawaona wanawake kama watu wa kuheshimiwa na kupendwa sana. Mkumbuke wanawake ndio mama zetu, walezi wetu na ndio nyumba zetu. Ridhika na mpenzi uliye naye, heshimu hisia zake na thamini mapenzi yake kwako na mpe ile kitu roho inapenda!

3 comments:

anne said...

jamaani mimi nashindwa kuelewa kwanini ni sisi tu wanawake tuwaheshimu wanaume?no no no ni pande zote mbili ndoa nikuheshimiana na kusaidiana katika kazi mbalimbali.zile zama za mamma zetu za kunyenyekea wanaume zimepitwa na wakati ukiniheshimu na mimi nitakuheshimu.ama sivyo talaka mbele

Anonymous said...

true..heshima ilikua wanaijua wale wazee wa zamani,yaani walikua wanaheshimiwa na wake zao na wao wanrudisha heshima basi mambo yanakua safi. sku hizi mwanume umuheshimu usimuheshimu mashetani yakimpanda atafanya atakalo.cha kufanya ni kuheshimu mumeo uki expect atfanya hivo na yeye ila huwezi kuendelea vumilia mtu ambaye hakuheshimu we kama mwanamke ,si lazima uwe sawa na yeye ila awe na ufahamu na aku appriciate we kama mwanamke na si vinginevyo. naomba kuwakilisha

Anonymous said...

Unatakiwa ujue mmeo ni mtu wa namna gani,Ukiheshimiwa na wewe pia unatoa heshima na kupigiana kelele hakubadilishi kitu kama umekosea unaona shida gani kuuliza kwa utaratibu?Upige kelele usipige haibadilishi kilichotea kwa hiyo tujifunze kujifahamu wenyewe,Maisha mazuri na kufurahia ni kuwa na usawa (mme na mke).