Tuesday, September 15, 2009

Chanjo mpya ya kansa ya mlango wa uzazi (Cervical Cancer) yagunduliwa



Mashosti wanasayansi hivi karibuni wametengeneza chanjo mpya ambayo inazuia virusi vinavyosababisha saratani ya mlango wa uzazi au cervical cancer.

Chanjo hiyo iliyotengenezwa na shirika la Glaxo SmithKline inaweza kuzuia aina mbalimbali za virusi kwa karibu asilimia 93, vinavyoweza kusababisha kensa ya mlango wa uzazi. Matumizi ya chanjo hiyo mpya hayana athari zozote mbaya muhimu kwa mtumiaji, isipokuwa maumivu kidogo na uvimbe sehemu inapochomwa dawa.

FDA imesema kuwa chanyo hiyo inaweza kutumiwa kwa wanawake wenye umri wa miaka 10 hadi 25.

Ugonjwa wa kansa ya mlango wa uzazi unasababishwa na virusi vya Papilomma (HPV) ambapo aina 15 za vijidudu hivyo huweza kusababisha ugonjwa huo. Kensa ya mlango wa uzazi ni kensa ya tano miongoni mwa saratani zinazosababisha vifo vya wanawake ulimwenguni, ambapo wanawake karibu 473,000 hupatwa ugonjwa huo kila mwaka.

Inasemekena kuwa karibu asilimia 85 ya vifo vya wanawake katika nchi zinazoendelea vinasababishwa na kensa ya mlango wa uzazi. Nchini Marekani pekee wanawake 11,999 hupata ugonjwa huo na serikali kutumia karibu dola bilioni 2 kwa ajili ya matibabu ya ugonjwa huo kwa mwaka.

http://www.presstv.ir/detail.aspx?id=105373§ionid=3510210

0 comments: