Wednesday, August 12, 2009

Kujifungua!



Hali ya kukosa taarifa hizo imewafanya vijana wengi kuwa na wasiwasi na kutokuwa na maandalizi ya kutosha kwa ajili ya kujifungua huko

Kutokana na uzoefu wa shughuli za uzazi, ni muhimu unapokaribia
kujifungua ukawa na mtu mzima anayeelewa taratibu zote ili aweze
kukusaidia na kukuelekeza mambo mbalimbali yanayoendana na uzazi.

Vijana wengi hawafahamu nini wanatakiwa kufanya wakati huo kutokana na
kukosa elimu ya malezi.

Ni muhimu kuwa na mama mtu mzima wakati ya kujifungua, kama vile mama
yako mzazi, dada au shangazi yako. Mama huyu anaweza kuwa na wewe
wakati wa uchungu hata kama muuguzi atakuwepo, kwani hawezi kuwa na
wewe wakati wote.

Wakati nchi nyingine zinaruhusu baba wa mtoto kuwa nawe wakati wa
kujifungua, hapa Tanzania utaratibu huu bado haujaingia. Amua unakotaka
kujifungulia mtoto wako na jinsi ya kufika hapo. Jiandae kwa kubeba
wembe, gloves, nguo kidogo za mtoto kama nepi, blanketi na khanga.

Ni muhimu kuwa na mtu mzima wa kunishauri na kunisaidia
wakati wa kujifungua. Mie nimeshamwita shangazi yangu akae na
mimi mpaka nitakapojifungua,anasema msichana Joyce ambaye ana mimba
ya miezi minane na nusu.

0 comments: