Monday, October 5, 2009

Unadhani kwanini wanawake wengi hutoka nje ya ndoa zao?
Shoga zangu nalazimika kuandika mada hii kutokana na maneno ambayo nimeyasikia hivi karibuni baada ya mwanamke mmoja maeneo ya Manzese ambaye ni mke wa mtu kufumwa na mumewe akijinafasi na ‘buzi’ gesti. Lakini cha ajabu licha ya mwanamke huyo kufumaniwa, maneno aliyoyatoa hayakuwa ya busara kwani nilimsikia akimwambia mumewe hivi, “ Ulidhani nimekuja kwako kula, hata kwetu nilikuwa nakula pia sasa kama hunitimizii ulifikiri mimi nitafanya nini zaidi ya kutafuta atakayeniridhisha, utalijua jiji”...


Nilishtuka kidogo kusikia maneno hayo lakini pia nikajiuliza sababu hasa za wanawake wengi siku hizi kufikia uamuzi wa kuwasaliti waume zao? Je, ni kutokana na kutoridhishana katika tendo la ndoa baina ya wanandoa? Kwa kweli mimi kama binadamu sikufurahishwa na maneno aliyoyatoa mwanamke yule kwa mume wake kwani naamini hakuwa sahihi.

Hivi kama mumeo hakuridhishi katika majambozi, suluhisho ni kutoka nje ya ndoa? Sidhani kwamba hayo ni maamuzi sahihi. Ila sasa baada ya tukio hilo nilikaa chini na kujaribu kufanya utafiti ili kubaini sababu ambazo zimekuwa zikisababisha wanawake wengi kuzisaliti ndoa zao. Huenda zikawepo nyingi lakini kwa haraka haraka nitazielezea tatu kuu.

Moja kati ya sababu hizo ni tamaa za kijinga zinazowatawala baadhi ya wanawake. Tamaa hasa ya pesa imekuwa ikiwashawishi baadhi ya wanawake kushindwa kujizuia kuwasaliti wapenzi wao. Kwa wale ambao wako kweye ndoa wakati mwingine hasa wanawake wasipopatiwa mahitaji yao muhimu na akatokea jamaa na kumhakikishia kumpatia kila anachotaka, wanakubali mara moja bila kujua kwamba wao ni wake za watu ama wapenzi wa watu na kujikuta wanajenga mazoea.

Lakini sasa cha kushangaza ni kwamba, wengine wanapatiwa kila kitu na waume zao lakini kinachotokea ni tamaa za kimwili tu ambazo zinawasumbua na kujikuta wanatafuta wanaume wengine ili mradi tu amepata ladha tofauti. Hili si kwa wanawake tu hata wanaume pia, unaweza kumkuta ana mke mzuri tu mwenye kila kigezo, lakini bado anakuwa na tamaa za kutafuta kimwana mwingine nje.

Pia wapo wanandoa ambao wanaishi maisha ya ajabu sana, yaani wanaishi katika ndoa lakini hawaaminiani kabisa, kila mtu anakuwa na wasiwasi juu ya mwenzake.

Itaendelea

2 comments:

Anonymous said...

Kwanza nakusalimia sana,mimi ni mwanaume wa miaka 25 nimeoa .Nina tatizo linalonichanganya sana nakunikosesha raha maishani mwangu,,mimi kipindi naowa mwaka 2004 nilikua na uume wangu wakutosha ,lakini tatizo nililonalo kwasasa kila kukicha uume wangu unyongonyea yani unapungua sana mpaka najiangalia nakua na oga.Sasa naomba ushauli kutoka kwako unisaidie njia ninayo weza kutumia ili niwe na uume wangu wazamani!! Nashukulu kwa majibu yako.

Anonymous said...

Asante kwa kuelimisha jamii,mie nacho hitaji nisaidie nfanye nini ili niwe angalau na maji ukeni,maana cku zote ni pakavu mno sana,hata mume aniandae vipi hamna,sijui ni tatizo gani msaada please,nyeti ni ndogo halafu haina maji ni mateso bola angalau maji yawepo hata ikiwa ndongo is ok.