Friday, October 30, 2009

Kutapika wakati wa ujauzito

Kutapika ni dalili inayojitokeza kwa mama mjamzito hasa kipindi cha awali ingawa tatizo la kutapika au kuhisi kichefuchefu linaweza kutokea katika maradhi mengine mbali na ujauzito.

Hali ya kutapika kwa mama mjamzito imegawanyika katika makundi mawili.Kwanza ni kichefuchefu na kutapika wakati wa kipindi cha mwanzo cha ujauzito ( Early pregnancy) na pili ni kipindi baada ya hicho cha awali (Late pregnancy).

Tukiingia kiundani kila kundi limegawanyika katika sehemu mbili.Ingawa hatutazama ndani zaidi,ila jambo la msingi ni kwamba katika hali ya awali (Early pregnancy),kutapika na hali ya kichefuchefu inaweza kuwa ya kawaida na isimletee shida kubwa mama (Morning sickness) na kutapika kidogo (emesis Gravidarum) na kuwa mgonjwa hata asiweze kufanya shughuli nyingine.

Mama huumwa hadi kuishiwa maji mwilini kwa kutema mate,kutapika na kushindwa kula na wakati mwingine hulazwa hospitali, hali hii huitwa kitalaam “Hyperemesis gravidarum.”

Yapo magonjwa mengine yanayosababisha kichefuchefu na kutapika ambayo yanaweza kumpata mama mjamzito na asiye mjamzito.

Magonjwa haya ni kama vile minyoo (Intestrial Infestations) maambukizi ya njia ya mkojo(Urinary Track infections),magonjwa ya ini(Hepatitis),ugonjwa wa kisukari (pale sukari inapokuwa juu) (Ketoacidosis of Diabetes),mkojo kuingia katika mfumo wa damu(uraemia),ugonjwa wa kidole tumbo (Appendicitis),vidonda vya tumbo (peptic ulcer) kuziba kwa tumbo (Intestnal obstruction) matatizo ya nyonga kifuko cha mayai (Twisted Ovarian cyst) na uvimbe katika kizazi (uterine fibroid).

Kutapika kunakoendelea wakati wa ujauzito (late pregnancy) huwa ni muendelezo wa hali hiyo.Tangu mwanzoni hali ya awali (Early pregnancy) hutokea mimba inapokuwa chini ya miezi minne lakini hii hali ya pili ‘Late pregnancy inatokea mimba inapokuwa zaidi ya miezi minne.Hapa mama huendelea tu kutapika na vilevile inahusiana na dalili za magonjwa mengine kama dalili za awali za kifafa cha mimba.

CHANZO CHA TATIZO

Mbali na maradhi mengine yanayohusiana na tatizo hili la kutapika wakati wa ujauzito,chanzo cha ugonjwa au tatizo hili ni pale mimba inapokuwa changa hadi baada ya kufikisha kati ya miezi mitatu na minne inakoma au ina weza kuendelea hadi miezi sita au hadi mama anapojifungua.

Tatizo hili linaweza kutokea katika mimba ya kwanza tu,wengine hutokea ya pili au wengine hutokea mimba zote.

Hali hii au tatizo hili linaweza kusababishwa na kuwepo kwa kiasi kikubwa cha hormone au kichocheo cha HCG mwilini au Human Chronic Gonadotrophin ambacho kikizidi kinakuwa sumu na kuanza kuchefua mwilini.

Hali ya kisaikolojia (psychogenic) pia huchangia kuamsha kichefuchefu kwa kutotamani baadhi ya vitu au vyakula au harufu.

Mama akiwa na hali hii hasa vyakula vya wanga hasa nyakati za usiku,asubuhi ataamka na njaa na kichefuchefu na kuanza kutapika na kuchoka.

Chakula cha wanga kama wali na ugali ni muhimu kwani vinatia nguvu na joto,vilevile uwepo wa vitamini B za kutosha nao husaidia sana.

Tatizo hili la kichefuchefu na kutapika pia huchangiwa na mzio (Allergies ) mbalimbali na tumbo kutofanya kazi vizuri (Decreased gastric motility).
NINI CHA KUFANYA

Hali hii ni tatizo sugu kwa baadhi ya akinamama kwani kila wapatapo mimba inakuwa shida.Tatizo hili linapoanza na ukawahi kumuona Daktari haliwezi kusumbua kwa kiasi kikubwa.

Mgonjwa atachunguzwa kama ana baadhi ya maradhi tuliyoyaeleza au kama kuna hitilafu zozote zilizosababishwa na ugonjwa.Mgonjwa baada ya uchunguzi atapatiwa tiba kadiri daktari atakavyoona inafaa.

Tiba mojawapo ni kuongezewa maji na dawa zitakazomsaidia kuondoa au kupunguza kasi ya kichefuchefu.

Mgonjwa akazane kula hasa vyakula vya jamii ya wanga pale hali inapokuwa nafuu,kunywa maji mengi na mara kwa mara ili hata kama hali hiyo itajirudia awe salama asisumbuke sana.

0 comments: