Tuesday, September 15, 2009

Kushare kitanda na laaziz sio kuzuri kwa afya


Wataalamu wanasema kulala kitanda kimoja na mpenzio si kuzuri kwa afya yako!

Wapenzi wanashauriwa kufikiria kulala vitanda tofauti, kwani kufanya hivyo ni vizuri kwa afya na uhusiano wao.

Mtaalamu wa masuala ya usingizi Dakta Neil Stanley amesema katika Warsha ya Sayansi ya Uingereza jinsi kulala kitanda kimoja wapenzi kunavyoweza kusababisha mapishano juu ya kukoroma na hata kugombaniana shuka usiku uliopita.

Utafiti umeonyesha kwamba, kwa wastani wapenzi wanakabiliwa kwa asilimia 50 na matatizo ya usingizi pale wanapolala kitanda kimoja.

Mtaalamu huyo ambaye analala mbali na mkewe, amesema kuwa kihistoria hatukutakiwa kulala kitanda kimoja. Ameelezea kuwa, desturi ya kisasa ya vitanda vya harusi ilianza tu wakati wa mapinduzi ya viwanda, ambapo watu walianza kuhamia kwenye miji na vitongoji vyenye misongamano ya watu na hapo ndipo walipojikuta wanakabiliwa na uhaba wa nafasi. Anaendelea kueleza kuwa, kabla ya kipindi cha Vitoria haikuwa imezoeleka kwa waliooana kulala pamoja.

Na wakati wa Urumi ya zamani, vitanda vya harusi vilikuwa ni sehemu ya kukutana kimwili lakini si kwa ajili ya kulala. Kwa hivyo Dkt Stanley amesema kuwa, watu hivi sasa wanatakiwa kufikiria kufanya hivyo.

Naye Dkt Robert Meodows ambaye ni mtaalamu wa elimu ya Sosholojia katika chuo kikuu cha Surrey anasema, watu wanafikiri wanalala vizuri zaidi wakati wakilala na wenzi wao, lakini ushahidi unaonyesha kinyume chake.

Uchunguzi uliofanywa kwa kuwashirikisha wapenzi 40 umeonyesha kuwa, wakati wenzi wakilala kitanda kimoja, na iwapo mmojawapo anahangaika hangaika wakati wa usingizi, kuna uwezekano kwa silimia 50, mwenzi wake akasumbuka kutokana na hali hiyo.

Uchunguzi huo umegundua kuwa, hata hivyo wapo wenzi wanaolala vitanda tofauti lakini wachache, huku wale walio kwenye umri wa miaka 40 au 50 kwa asilimia 8 hulala vyumba tofauti.

1 comments:

mumyhery said...

mm mhuu, kila mtu na kitanda chake!!! ni kweli lakini bado naguna