Thursday, July 30, 2009

Je Dawa za minyoo zinatoa mimba??


Wapendwa,
poleni sana na kazi za ujenzi wa taifa na kujitafutia mkate wa kila siku.
Ninaishi na girl friend wangu ambaye siku ni mfanyakazi wa kampuni moja jijini.

Siku kadhaa zilizopita aliniambia kuwa amepata ujauzito na anahisi una umri wa mwezi mmoja.
binafsi nilifurahishwa sana na taarifa hizo kwani sasa ka umri kamekimbia na sina hata mtoto wa kusingiziwa. Lakini mwenzangu hakuwa anaonekana amefurahishwa na jambo hilo la ujauzito wake na akanishauri kuwa atoe, nikagoma.
leo ameamka mapema sana na ameniaga kuwa anaenda kununua dawa za minyoo zinazoitwa Zentel.
Je hizo dawa haziwezi kuharibu ujauzito ?
NA NI NINI MADHARA YA DAWA HIZO KWA MTU MWENYE UJAUZITO MCHANGA KAMA HUO ?

6 comments:

........................... said...

this is very interesting my dear, amekwambia kuwa ana mimba lakini akakushauri kuwa anataka kutoa. Hivi kutoa si ndio abortion? au nakosea? What does this mean so far? Sitaki kukukatisha tamaa lakini chunguza kwanza kuhusiana na uhalali wa hiyo mimba kama ni ya kwako au la. Kwa fikira zangu nilitegemea huyu GF wako angefurahi kusikia wewe umeipokea hiyo mimba kwa moyo mkunjufu

........................... said...

pole sana mkuu nilishawahi kukutana na situation kama hiyo.mchumba wangu alikuwa na mimba na hakuwa tayari kuzaa,nilijitahidi sana kumconvince yeye alichokuwa anataka ni abortion tu.Sababu nilikuwa nahitaji mtoto tena wa kwanza mda wote nilikuwa na hofu ya mimba kutolewa,hata alipokuwa akiniaga anakwenda mjini nilichokuwa nawaza ni hicho tu,aliyenisaidia alikuwa ni bestfriend wake ambaye alimwambia ukitoa mimba bila ruhusa ya mwenye mimba waweza kufa na akamwambia watu wengine kwenye koo zao mimba zao huwa hazitoki ukizitoa waweza kufa hivyo itabidi ushauriane na mwenye mimba.Alipokuja kwangu alijifanya kunitega kwa maswali kama kwetu watu wanakufaga kwa kutoa mimba.sababu best yake alishaniambia mchezo wote aaah kwangu ilikuwa kama kuua tembo kwa ubua.nilimpa takwim za uongo tena huku machozi yakinilengalenga.now i am a dad of three months healthier baby!!.Dawa za minyoo hazitoi mimba ila kwa ushauri Hasinywe dawa yoyote bila ushauri wa daktari sababu mimba ni special case na hata wauza madawa hawakubali kutoa dawa kwa wajawazito bila cheti labda isiyoonekana kama ya girlfriend wako.

........................... said...

Hizo dawa zimeandikwa kuwa asitumie mama mja mzito. Kwamba zinatoa mimba au kuharibu sijui. Ila wanawake wengi hujaribu kutoa mimba kwa njia za hatari hatari sana kwa sababu hawana elimu ya uzazi. Matokeo yake huishia na madhara kibao hadi kifo kwa wengine. Kama mimba haitakiwi si aende kunakohusika ajieleze apewe ushauri nasaha?

........................... said...

kuwa makini sana na huyo rafiki yako,kama ulivyo sema yeye akufurahia icho kitendo cha yeye kupata ujauzito na akakushauri mkaitoe,naona hapo kuna kamchezo anachotaka kukuchezea,anaweza kutumia hiyo dawa alafu akuambie mimba imearibika kutokana na hiyo dawa.Ushauri: mwambie asitumie hiyo dawa kwani mimba yake bado ni changa,na anapaswa kutumia dawa kutokana na ushauri wa daktari tu na sio vinginevyo.

Kama anahisi ana minyoo mpeleke hospitali mwenyewe akachekiwe.kitu kingine mkuu ebu jaribu kumchunguza kama yupo tayari kukuzalia mtoto maana usije kuta huyo msichana yupo na wewe tu kwa sababu zake binafsi na hana lengo lolote na wewe.
Swala la kuzaa mkuu sio la kukurupuka tu na kuchukua maamuzi ya ghafla,kaa nae chini mzungu mzie jambo hilo kwa makini.

Anonymous said...

Kiukweli nilishawahi kusikia mimba ikiwa ndogo ndio inaweza kuharibika lkn kwa mimba kubwa sidhani kama kuna tatizo...ni maoni tu lakini hayo ila ni vyema ukapata ushaui wa daktari shosti

Anonymous said...

Dawa ya minyoo haitoi mimba, huyo dada anajisumbua tu. Mimi pia niliwahi kunywa dawa ya minyoo nikiwa na mimba changa kabisa, na wala haikutoka wala nini, na sasa hivi nina mtoto wangu yuko fit na salama. Ila kama ataamua kubugia kwa kujioverdose kama sumu, hapo dawa yoyote ile yaweza kuwa na madhara kwake.

Wakati mwingine hata mke ndani ya ndoa anakuwa hayuko tayari kubeba mimba, kutokana na depression anayopata kutokana na change of hormones. Sasa unachotakiwa kufanya ni kuongea na huyo dada ujue yuko kwenye situation gani kisaikolojia kuhusu hiyo mimba. Na wewe uko tayari kumsapoti kwa kiasi gani, maana kama hamna committment yoyote ambayo iko fixed, wakati mwingine huwafanya wasichana wasite kuzaa, wakihofu hatima yao na ya hao watoto watakaowazaa. Wanawake wako sensitive sana kuhusu kuzaa nje ya ndoa kwani ukishamtema wewe kupata mwanamume mwingine ambao ataaccept kuwa alishazaa na ana mtoto huwa ni vigumu kidogo, lakini kwa wanaume wao hata kama amezaa na wanawake wa tatu au wanne tofauti hiyo haina shida anaweza kuanza mahusiano mapya na mwanamke yoyote anapojisikia.