Monday, February 1, 2010

Jipambe ili kuongeza mvuto kwa mumeo!


Ni wiki nyingine ndani ya kona ya dondoo za mwanamke , kona inayokuletea mambo mbalimbali ambayo mwanamke anatakiwa kufanya katika nyumba au jamii inayomzunguka , nawashukuru wasomaji wangu ambao husoma makala na kuzifurahia kwani naona ni jinsi gani mnanikubali na ujumbe unawafikia......


Nisiongee mengi kuwachosha leo ndani ya kona hii tutaongelea jinsi ya kumvutia mumeo wakati wote na kuepuka kwenda nje ya ndoa , nasema hivyo kwani akina mama au dada wengi wakishaolewa na kupata watoto hujisahau na kujali majukumu mengine na kujisahau kama hapo awali alikuwa akijipendezesha kwa hali na mali ili kumvutia mwanaume huyo.

Sisemi eti usimpende mtoto hapana lakini kila mtu awe na nafasi yake kwani mara nyingi kwa kufanya hivyo wanaume huwaonea wivu watoto na wakati mwingine hata kuchukia ujio wao kwani matunzo kwao na kuwajali waume zao hupungua na kutothaminika tena.

Fanya hivi:
Mpe nafasi mtoto na baba kwa wakati wake, hii husaidia hata kujenga ukaribu kwa baba na mtoto nasema hivyo nikimaanisha kuwa ,usimsahau baba (mumeo) pale anapohitaji huduma zote za awali ambazo ulikuwa ukimpa kabla ya kujifungua kama vile kumpokea pindi anaporudi kazini, maandalizi mazuri wakati wa kumuandalia msosi, mapenzi motomto ya awali na vinginevyo anavyopaswa kupewa mwanaume katika ndoa yake, naye mpe nafasi yake ili kuilinda ndoa kwani kwa kutompa nafasi itachangia kwenda kutafuta huduma hizo nje.

Jipambe:
Jipambe na kujiweka katika hali nzuri ili kumuweka karibu mumeo kama ilivyokuwa kabla ya kupata mtoto, nasema hivyo kwani utakuta muda mwingi mama ananuka maziwa anajiweka katika hali ya kuchakaa ukiuliza nini utaambiwa eti analea si hivyo utamchosha mume na kuanza kwenda kutafuta mwanamke ambaye anajipenda na kutaka kupendeza wakati wote.

Yawezekana si mzuri kama ulivyo wewe lakini kwasababu umejiweka katika hali ya kuchakaa ‘rafu’ atakushinda tu na kumvutia huyo mumeo .
Kumbuka:

Kumbuka kuvaa nguo zinazomvutia mumeo kabla ya kuwa mjamzito na kuzaa , kumbuka siku ya kwanza ulimvutia kwa kitu gani, ukiweka kumbukumbu kichwani kwa mambo hayo na kuyafanya pale unapomaliza kujifungua utampa nafasi mumeo ya kukuweka karibu na kukutamani kila wakati, hata pale atakapokuwa mbali nawe atatamani kukuona , hiyo itamrudisha mumeo nyumbani haraka kwani hatakumbuka kutoka wakati anayoyafuata nje nawe unayafanya ndani.

Kuzaa si suluhisho:
Wanawake wengi wakishazaa wanadhani kuwa kwa kumpatia mume mtoto basi atamuheshimu, atampenda zaidi ya mara ya kwanza alipokutana naye kabla ya kumuoa na akiaminikuwa hawezi tena kutoka nje kwani atakuwa amefurahi kuletewa mtoto , huu si ukweli.

Mtoto ni zawadi kubwa na chachu ya kudumisha ndoa yako kwa mumeo na wewe mwenyewe lakini haimzuii kukumbuka mambo uliyokuwa ukimfanyia hapo nyuma.

0 comments: