Monday, November 30, 2009

Mjini vs kijijini wapi kuna wasichana bora?


Nina furaha sana kukutana nanyi tena leo. Ni imani yangu kwamba mtakuwa wazima wa afya njema na mnaendelea vyema na majukumu yenu ya kila siku...

Karibuni sana katika uwanja wetu huu ambao hutupa nafasi ya kubadilishana mawazo juu ya haya mambo ya mapenzi. Kila mmoja anaweza kuwaza awezavyo, maana kila mtu ana uhuru wa kuwaza na ikiwezekana kutoa hisia zake.

Mimi pia nitatoa hisia zangu kama, nitaeleza ninachokiamini , halafu mwisho wa siku, wewe msomaji unayesoma hapa utapata wasaa wa kutoa maoni yako.

Huu ni mjadala wa siku nyingi sana, nafikiri ni kuanzia vizazi na vizazi, watu wanawaza, wanauliza, ni mwanamke gani hasa anafaa kuwa mke bora ndani ya nyumba? Ni yule wa kijijini au wa mjini? Kwanza nitaanza kwa kuwachambua wanawake hawa waliokulia katika mazingira mawili tofauti kabla ya kuendelea na uchambuzi zaidi.

WA KIJIJINI!
Je, ni kweli kwamba mwanamke wa kijijini ni bora zaidi kuliko wa mjini? Wapo wanaofikiria hivyo, lakini hapa nitakupa mazuri na mabaya yao, japo kwa uchache tu ambayo yatakupa mwanga wa uchaguzi wa mke bora.

*Mazuri yake
Haya ni baadhi ya mambo mazuri ambayo mwanamke wa kijijini anakuwa nayo. Mwanamke huyu anaelezwa kuwa na heshima kupindukia, siyo mkaidi, muelewa na mwenye heshima sana kwa mumewe.

Hana makuu, hapendi starehe, anajali familia yake, ndugu wa mumewe na hata marafiki wa karibu na mume wake. Anajua shughuli za nyumbani kama mke, lakini pia ni mtafutaji mzuri kwani mara zote hujishughulisha na biashara ndogo ndogo au kilimo.

Ni mwepesi kuelewa mambo, hasa kama anakatazwa au kuonywa. Anajua nafasi yake kama mke na ‘anacheza’ ipasavyo katika nafasi hiyo. Anaweza kuishi maisha ya aina yoyote.

*Mabaya
Inaelezwa kwamba, asilimia kubwa ya wanawake wa vijijini hawajaenda shule! Wengi huishia darasa la saba na kuolewa au kubaki nyumbani. Hili huvumbua kasoro nyingi nyuma yao, lakini kubwa zaidi anakuwa hana ufahamu wa mambo mengi.

Hajui dunia inaendaje, mawazo yake siyo endelevu na siyo mapana. Hana mipango ya muda mrefu, anamtegemea zaidi mumewe kwa kila kitu. Baadhi yao huamini kuolewa ndiyo kila kitu na mume ndiyo kila kitu katika nyumba.

Kwamba anaweza kufanyiwa kila kitu na mumewe kwasababu eti ni mume! Siyo mwepesi wa kugundua makosa au matatizo haraka. Ni rahisi kufanya jambo baya na kung’amua baadaye sana ubaya wa jambo alilolifanya.

Siyo mjanja, ni mzito kifikra. Muoga kujifunza. Baadhi yao hupelekwa unyagoni ambapo hufundwa na kuelekezwa anayotakiwa kuyafanya kama mwanamke. Mara nyingi hupelekwa huko akiwa na umri wa kuanzia miaka 13-15, akitoka huko anaamini tayari yeye ni mtu mzima!

Anaanza kufanyia mazoezi aliyofundishwa! Mafunzo yanayotolewa huko yanadaiwa kuwa si mazuri sana, kwani mtoto hufundwa mambo mazito ambayo anapaswa kufundwa mwanamke ambaye anajiandaa kuingia kwenye ndoa.

Kuharibikiwa huku mapema, wakati mwingine kunaweza kumuathiri hata anapokuwa mtu mzima na familia yake.

Haya ndiyo baadhi ya mabaya na mazuri ya mwanamke wa kijijini. Hii ni mada pana, ambayo inahitaji utulivu wa fikra ili kuweza kupata ujumbe sahihi uliolengwa.

Katika toleo la Jumamosi, nitamchambua mwanamke wa mjini, kabla ya kugeukia kwenye chimbuchimbu zaidi ya kufahamu ni yupi bora zaidi kati ya hawa? Usikose.

2 comments:

Bennet said...

Wakijijini ukimleta mjini halafu akazibuka inakuwa balaa yaani kama mbwa mwenye kichaa kakata mnyororo anataka kung'ata kila mtu
Basi na huyu wa kijijini naye atataka kujifanya kila kitu anajua, na asionekane yeye mshamba na hapo ndio anapoharibu, anagalia nikusaidiaje ya Prof Jay
Lakini kama mwanamke amezaliwa na kukulia kijijini halafu katika kusoma kwake akaishia mjini anakuwa mzuri sana watabia kwa sababu ana kuwa chotara wa mazingira yote mawili

Anonymous said...

wa kijijini. hawa wa mjini takataka tupu. ili kuona matako ya mwanamke wa kijijini unatakiwa kuvua chupi yake lakini ili kuona chupi ya mwanamke wa mjini unatakiwa utenganishe matako yake (G-strings)