Monday, October 19, 2009

Kwanini hufurahii tendo la ndoa?


Kila mada inapotoka nakutana na maswali mengi sana, huwa nayachuja, najaribu kujibu machache.

Lakini kuna maswali mengine huwa yana uzito zaidi, hata kama nikiamua kumjibu muhusika mwenyewe, naona kabisa kuna wasomaji wengine wengine wanaweza kuwa na tatizo kama hilo, lakini wameshindwa kuuliza.

Hiyo ndiyo sababu iliyonifanya leo nijibu baadhi ya maswali ya wasomaji wangu kwenye nikiamini majibu yatakuwa msaada hata kwa wengine wenye matatizo kama hayo. Tuanze na hili hapa chini.

SIFURAHII TENDO LA NDOA!
Pole na majukumu yako ya kila siku. Ninalo tatizo moja kubwa linalonisumbua, yaani ninapokuwa na mpenzi wangu faragha sifurahii kabisa mapenzi. Kuna rafiki yangu niliwahi kumuuliza akaniambia labda ni kutokana na kutoniandaa kabla ya tendo lakini ukweli ni kwamba kaka Jose mpenzi wangu huwa ananiandaa vya kutosha, sasa sijui tatizo ni nini? Nimehangaika sana na tatizo hili. Naomba msaada wako. Shose, Dodoma.

Jibu: Pole sana dada Shose, tatizo lako limewakumba wengi, kwanza hujaniambia umri wako, matatizo haya mara nyingi huwatokea wasichana wenye umri mdogo ambao hawajapevuka, pia wakati mwingine unapaswa kuweka mawazo yako katika tendo lenyewe unapokuwa na mpenzi wako.

Pili, mara nyingi wanaoshindwa kufurahia tendo la ndoa inatokana na mapenzi juu ya yule ampendaye. Hivyo basi jaribu kuangalia kiasi gani unavyompenda mpenzi wako, wakati mwingine unaweza kuwa una mawazo mengi.

Hakikisha unakuwa na mwenzi ambaye moyo wako umeridhia kuwa naye, weka akili yako kwenye tendo wakati unapokuwa naye faragha. Epeka kufikiria mtu aliyekuudhi au jinsi ulivyopata matatizo kazini mchana wa siku hiyo.

Kuwa mtulivu kwa kiwango cha mwisho. Wakati mwingine inawezekana mwanaume wako wa kwanza kufanya naye mapenzi, hakukuandaa vya kutosha na hivyo kukuumiza na hivyo kila mwanaume kwako kuhisi anakuumiza.

Kama ndivyo, hili ni tatizo la Kisaikolojia, ambalo linahitaji tiba ya ushauri wa karibu zaidi kuliko dawa! Onana na Mwanasaikolojia aliye karibu na wewe au Mtaalam wa Afya ya Uzazi wa Mwanamke. Vizuri zaidi kuonana na Wataalamu wa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma (General Hospital) au Rufaa ambao watakupa msaada zaidi. Kufurahia mapenzi ni haki ya kila binadamu aliyekamilika.

DEMU KANIDATISHA LAKINI DOMOZEGE!
Shikamoo kaka Shaluwa. Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 17, tatizo linalonisumbua ni aibu. Kuna msichana nampenda sana kuanzia nikiwa darasa la sita hadi sasa nipo kidato cha pili.

Ukweli ni kwamba nampenda sana lakini nashindwa kumweleza yaani nina aibu sana. Naomba msaada wako kaka yangu. Natamani sana na mimi kuwa na msichana wangu, lakini domo langu zege jamani! Nisaidie bro. Nakutegemea. Mwenye matatizo, Dar.

Jibu: Marhaba mdogo wangu mwenye matatizo. Pole sana kwa yote lakini nashukuru sana una aibu na ninakuombea uendelee kuwa nazo hadi pale utakapokuwa mkubwa. Kwa umri wako lazima uwe na aibu, hata hivyo huu sio muda wako wa kuhangaika na mapenzi.

Mtoto wa miaka 17, utamudu kuwa na mpenzi kweli? Mpenzi wako kwa sasa ni shule mdogo wangu na siyo ngono. Achana kabisa na mambo ya mapenzi maana yatakuchanganya na utashindwa kufanya vizuri darasani.

Tengeneza maisha yako kwanza kisha mambo mengine yatakuja baadaye, mapenzi hayana maana ikiwa bado hujajua dira ya maisha yako. Soma kwanza, mapenzi utayakuta baadaye. Naamini umenielewa. Masomo mema.

HUYU NAYE VIPI, HAPOKEI SIMU YANGU...
Hi bro! Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 28, nina mpenzi wangu ninayempenda sana lakini kweli amekuwa akiniweka katika wakati mgumu sana kutokana na mambo yake. Kwanza siku hizi amebadilika sana, nikimpigia simu hapokei na hata akipokea huwa anachelewa sana, wakati mwingine anaweza kuzima simu hata siku tatu mfululizo. Nikimuandikia meseji hajibu na ukimuuliza anasema ana kazi nyingi ndiyo maana anashindwa kupokea simu yangu. Je, ananipenda kweli huyu? Naomba unishauri wako.

Jibu: Pole sana mdogo wangu, kwanza naomba ufahamu tatizo hili ni sugu kwa wapenzi wengi wenye mapenzi ya ‘filamu’, wanaojua kuigiza mapenzi lakini hawana mapenzi ya dhati ndani mwao.

Kwa tabia hiyo inaonekana mwanaume unayempenda atakutesa sana maishani mwako, inasikitisha unaposema mpenzi halafu anashindwa kukujali. Mwanaume huyu hajui nini maana ya mpenzi, siku zote mpenzi hatakiwi kuumizwa na anapoumizwa basi anaomba msamaha.

Jaribu kumchunguza taratibu utapata ukweli, hata kama ni ‘ubize’ lazima awasiliane na wewe. Wanaume wengi wamekuwa wakiwaumiza sana wapenzi wao ingawa pia wapo wasichana wenye tabia hizi, utakapogundua mpenzi wako ana uhusiano na mwanamke mwingine ni vema umwache kwasababu utakapofunga ndoa anaweza kukutesa zaidi ya hapo.

Bila shaka mliouliza maswali na hata wale ambao hamjauliza, mmenufaika na majibu haya. Ahsanteni.

0 comments: