Thursday, October 15, 2009

Hivi ndivyo unavyoweza kuipata raha ya majambozi

Wanawake wengi hushindwa kuwaeleza wapenzi wao nini hasa huhitaji pindi wanapokuwa kwenye sita kwa sita na hii inaweza ikawa ni kwa sababu ya kushindwa kujiamini kama siyo uelewa mdogo wa vionjo vya majambozi, sababu nyingine ni kuwa wanawake wengi huamini kuwa wanaume huzisoma hisia za wapenzi wao pindi wanapowaandaa na mpambano jambo ambalo si kweli kwani wengi wao ni wabinafsi yaani gari ikikubali starta tu huanza safari hata bila kupima oil wala kuangalia kama maji yanatosha kwa kuianzisha safari.

Dada yangu huna sababu ya kusimuliwa kila siku raha ya mechi ni nini kam hujui mimi nakwambia ni bao! kama huamini ngoja Taifa Stars ifanye kweli kwenye mechi ya marudiano na Cameroon usikiye hizo kelele za Watanzania, hivyo ukitaka kufurahia mapenzi na mwenza wako faragha lazima ujue nini hasa hukupandisha mzuka wa kulianzisha kunako sita kwa sita.

Dada zangu, wadogo sina budi kuwaasa haya yafuatayo ili ukiwa faragha upagawe na mwenza wako siyo kila siku wewe uwe msindikizaji tu. Sasa endelea...

Jitowe hofu; endapo utaingia kwenye uwanja wa raha ukiwa na hofu ya aina yoyote amini hutaweza kuweka mawazo yako katika kile mnachokifanya, badala yake utakuwa ukiwaza jambo linalokutatiza. Mfano kama unawasiwasi na harufu inayotoka kwenye mambo yetu yale huna budi kuhakikisha unaingia bafuni na kujiweka safi kabla ya kuingia faragha na wapo wale wenzangu ambao wakiguswa vema kwenye maeneo yenye kumpandisha midadi tu basi haja huwatoka,sasa kama nawe ni miongoni chukua taadhali mapema kwa kwenda kujisaidia.

Yatambuwe maeneo ambayo ukiguswa mzuka unakupanda; hakika huwezi kufurahia majambozi kama wewe mwenye hujui maeneo gani hasa mzee akiyatumia vizuri katika maandalizai ya mpambano atakupagawisha. Kama hujui maeneo yapi hasa hukupa hamasa ya kutaka kufanya mapenzi basi jifanyie utafiti leo na ukibaini yafanyiye mazoezi ya vitendo na mwenza wako na kama unashindwa kuyatambua tuwasiliane.

Kamwe usimtegemee mwanaume pekee kuamsha hisia zako uwapo faragha; wanaume si wasomaji wazuri wa hisia hivyo ni rahisi kwao kutobaini nini hasa kinachoamsha hisia zako ya kutaka kula sukariguru hivyo kama unajua usisite kumuongoza kwenye maeneo hayo ili aweze kukupagawisha vinginevyo kila siku utabaki kusikia 'oh mapenzi raha bwana' usilaze damu jitoe akili mueleze bayana nini unataka akufanyiye uipate raha ambayo wengi wanadai kuipata toka kwa wenza wao.

0 comments: