Tuesday, September 8, 2009

Mazoezi ya kuondoa ndambi (Tumbo)


kiwa wewe hujawahi kuzaa nitakushauri ufanye mazoezi ya kukimbia kisha malizia na “sit-ups” mia moja kwamba hamsini asubuhi na hamsini jioni. Hakikisha unaanza mazoezi asubuhi kabla hujala kitu kinaitwa kifungua kinywa (muda mzuri kuanza ni alfajiri au asubuhi kati ya saa moja na mbili) na muda mzuri kwa mazoezi jioni ni kuanzia saa kumi, kumi namoja na saa moja kabla hujala mlo wa jioni.

Siku ya kwanza itakuwa ngumu siku ya pili mpaka wiki utapatwa na maumivu ya misuli sehemu ya tumbo, hiyo ikitokea inamaana kuwa misuli inafanya kazi na hupaswi kupumzika au kuacha

Kwa wale mama wapya; ndio umejifungua hivi karibuni ni vema ukafuata maelekezo ya Mkunga wako na watu wengine lakini kumbuka tu kuwa unakula chakula cha kukutosha wewe na sio kula kwa ajili yako na mtoto (kiasi cha maziwa kinatoka kilekile hata kama utakula mlo wa watu wanne).

Unachopaswa kuzingatia ni kula mlo kamili wenye virutubishao vyote (balance diet) kama vile wanga, mafuta, protini n.k. Pia kumbuka na kukaza tumbo lako kwa kulifunga khanga nyepesi au kitambaa chepesi ili kusaidia kurudisha tumbo lako la uzazi na kuwa kama lilivyokuwa awali kabla hujawa mjamzito.

Nashauri mazoezi haya yafanywe wiki sita au mtoto anapotoka Arobaini (kwa waislamu) baada ya kujifungua kwa njia ya kawaida na sivinginevyo, vilevile yafanywe hatua kwa hatua. Mfano leo unafanya hatua ya kwanza, kesho ya pili n.k, hivyo ni vyema kama utaandaa ratiba yako ambayo itakusaidia au kukumbusha zoezi linalofuata .

*Hatua ya kwanza ni zoezi liitwalo “maombi”na lina sehemu mbili( hukaza misuli ya tumbo na kuondoa uvimbe).

Mosi, lala chali, kunja miguu yako, hakikisha kuwa unyayo uko sambamba na sakafu. Tenganisha kidogo mapaja yako na uweke mikono yako katikati huku viganja vikiwa vimekutana, kasha nyanyua kichwa na sehemuya juu kidogo ya kifua na kurudi chini mara kumi.

Pili, ukiwa umelala hivyohivyo jitahidi kuinua kichwa hadi sehemu ya mgongo na kurudi chini mara kumi.

*Hatua ya pili nayo imegawanyika katika sehemu mbili na zoezi lenyewe linaitwa “uti” (huimarisha mgongo, hupunguza tumbo, makalio na mapaja).

Mosi, lala chali,kunja miguu yako, smbaza mikono yako huku na huko na viganja vyako vikiangalia juu.

Hakikisha miguu na magoti vimetengana kama inchi tano hivi. Vuta pumzi (usitoe) geuza kichwa chako upande wa kushoto , huku magoti, miguu na makalio vikiwa upande wa kulia. Kaa hivyo kwa dakika tatu.

Pili, Rudisha kichwa mahali kilipokuwa mwanzo na upumue, rudia tena kama awali kadri uwezavyo lakini kumbuka kubana pumzi na kutoa pumzi sehemu ya pili ya zoezi hili.

*Hatua ya tatu ni zoezi liitwalo “kunja nyonga” vilevile limegawanyika katika sehemu mbili na hukaza misuli ya tumbo na kulipunguza .

Mosi, lala chali, inua miguu juu huku mikono yako ikiwa huku na huko na viganja vikiangalia juu, kaa hivyo kwa dakika moja na kisha nenda sehemu ya pili.

Pili, Peleka miguu yako (ikwa imeinuka juu) hadi kwenye kichwa na uhakikishe kuwa makalio yako yameinuka na ukae hivyo kwa dakika mbili kisha rudisha miguu yako chini na urudie tena mara ishirini.

2 comments:

Anonymous said...

Ma dear huwa napenda kusoma mada zako, ila kila nikifungua nikikuta vimaandish vilivyo vidogo napata uvivu! unaweza kuweka font size kubwa kidogo mamy? ni ombi!

Anonymous said...

Asante sana dada kwa mada zako nzuri za kutuelimisha,swali langu ni mfano sisi ambao hatujazaa mfano mimi napenda umbo langu but the only problem ni tumbo je haya mazoezi uliotuambia yanapunguza tumbo tuu au na mwili mzima coz i'd love kupungua tumbo TUU.

Thanks.