Tuesday, September 1, 2009

KUZUIA MIMBA KWA KUTUMIA KALENDA


Kwanza nataka niwaeleze wadau juu ya athari za vidonge vya kuzuia mimba:

Wanawake wengi hujikuta wanakumbwa na machafuko ya tumbo au kutapika wakati wa asubuhi, kuvimba matiti kama siyo kukumbwa na dalili za ujauzito mara wanapoanza kutumia vidonge kwa mara ya kwanza!Hii husababishwa na vidonge hivyo ambavyo vina hormones zile zile ambazo mwanamke huzitia kwenye damu wakati akiwa na mimba. Hata hivyo wataalam wanasema kuwa dalili hizi hufikia kikomo baada ya miezi kati ya 2 hadi 3.

Sambamba na hilo watumiaji wengine wavidonge hutokwa na damu nyingi wakati wakiwa kwenye siku zao.

Athari kubwa anayoweza kuzipata mtumiaji wa vidonge vya kuzuia mimba ni kuganda kwa damu kwenye moyo, mapafu au ubongo!

Wadau naomba muelewe kuwa kwa wanawake wengine mimba pamoja na kutumia vidonge vya kuzuia mimba vina hatari kubwa zaidi kwao. Hivyo basi wanawake hawa ni lazima watumie njia zingine za kuzuia mimba!

Baada ya kutanabaisha hayo naomba sasa nimjibu dada yangu jinsi yakutumia kalenda kujikinga na mimba!

Njia hii haina uhakika sana wa kuzuia mimba, lakini ni nzuri kwa sababu haigharimu chochote.Njia hii huwafaa zaidi wanawake amabo taratibu za siku zao za kwenda mwezini ni kawaida mara moja kila baada ya siku 28, na ili iweze kuzaa matunda, njii hii huhitaji mtumiaji awe tayari kukaa bila kukutana kimwili kwa muda wa wiki moja kila mwezi!

Kwa kawaida kuna siku 8 tu kila mwezi ambazo mwanamke anaweza kupata mimba ambapo siku hizi zipo katikati ya siku zake za kwenda mwezini, na huanza siku 10 baada ya siku ya kwanza ya kupata damu ya hedhi. Hivyo basi ikiwa mwanamke yoyote hataki kupata mimba ni lazima aache kukutana na mwanaume kwenye siku hizi 8! Naamini hili linawezekana kwani siku nyingine zilizobakia wapendanao wanaweza kujiachia kama kawaida kwani hakuna uwezekano wa mwanamke kushika mimba!

Ili kuepukana na kutatanikiwa, ni lazima mwanamke aonyeshe kwenye kalenda zile siku ambzo hatakiwi kukutana na mwanaume. Hapa inaweza kuwa ngumu kuchora kalenda ya ukutani kwa kuwa inatumiwa na wengi lakini ni rahisi kutekeleza hili kwa kutafuta pocket kalenda [kijikalenda ambacho waweza kiweka kwenye pochi yako]

Kwa mfano: Unaingia kwenye siku zako tarehe 5 Desemba, weka alama kwenye tarehe hiyo kisha hesabu siku 10 na baada ya hapo pigia msitari siku 8 zinazofuata!

Angalia mfano huu:-

Kumbuka siku hizo nane utakazozipigia msitari ni hatari kwani ukikutana na kidume tu na kushiriki ngono bila kutumia kondom utashika mimba, hivyo ni vema usikutane na mwanaume hata kidogo, yani epuka hata akikubembeleza na lugha laini kuwa nitapizia nje sweetie, sijui nini na nini kama hataki tumia kondom kataa kwani kupizia nje ni bahati nasibu hasa pale mwanamke anapoamua kumpa mwanaume maujuzi ya kabatini ambayo ni adimu, yaani mwanaume hupewa kwa sababu maalum tu hali inayomfanya apagawe kwa huba na hivyo huweza msababisha ashindwe kupiziza nje!

Nimalize kwa kusema kuwa, mwanamke anapaswa kuendelea na utaratibu huu kila mwezi lakini akumbuke kuwa, njii haina uhakika sana mbaka itumiwe sambamba na njia nyingi9ne kwama vile kondom.

18 comments:

Anonymous said...

asante da Joan kwa kutuelimisha ila kuna wengine jamani mizunguko yetu mirefu mpaka basi,kwa mfano ukiingia mwezini tarehe 21 mwezi wa saba,mwezi unaofuatia unaweza pata kwenye tarehe 31 mwezi wa nane au husipate kabisa mpaka mwezi mwingine tena na uwa mara kwa mara sio kusema mabadiliko ya khali ya hewa hapana ni kila mwezi hii itakuwa nini? Na je njia hii inaweza kuwa salama kwetu.

Anonymous said...

zeze mbona mimi cjaelewa? uaweza kuelewesha kwa njia nyingine zaidi?

Anonymous said...

Unachosema zeze ni kweli mm katika maisha yangu huwa natumia calenda nasijawaikusa kizembe,ingawa tarehe zangu zinabadilika km alivyosema huyo dada hapo juu,mm nakumbuka tulijifunza nikiwa oleve mbaka sasa ninatumia njia hiyo hiyo.

kwa mfano

mm this month nimeingia tarehe 17 sikuzangu za period ni 7 so kuanzia tarehe 17 -23 ni period na kuanzia tarehe 24-30 naweka ni hatari maana hujuinisiku gani yai linashuka.then siku zingine zote ni safe day i hope sikombali sana wewe zeze

Anonymous said...

me nataka nipate mimba je nisiku gani nzuri kumake love? mwezi wa 8 nimeblid tarehe 22/25

Anonymous said...

Mimi pia nataka kupata mimba lakini sijui ni siku gani ni nzuri,mfano mimi huwa napata hedhi kuanzia tarehe 3-8,je ni siku ya ngapi naweza pata mimba? alafu ili kujua umepata mimba dalili zinaanza kujitokeza baada ya Muda Gani?
Pliz naomba unijibu maswali yangu.

Anonymous said...

mm nadhani kwa ambaye ajaelewa zaidi ni kwamba siku hunayoanza kuona hedhianza kuhesabu 1-14 alafu toa siku 4 nyuma na 4mbele zilizobaki ni self kuendelea

Anonymous said...

asante mdada ila mi bado nachanganya mambo kuhusu hii njia,kama mimi nina mzunguko unaobadilika kila mwezi mara siku 21 au 23 au 25 embu nisaidieni nikitumia njia hiyo ya kuhesabu kumi na kukata nane yani tayari nimeshakaribia period tena na niliambiwa na one of my friend 3days kabla ya period ni hatari...nisaidieni manake nipo kwa giza kabisa

Anonymous said...

Kuna some website zinaelezea how to get pregnant..try www.ovulation- calender.net unaweka the last date of ur period(kama period zako zilianza tarehe 2/10/09 na mzunguko wako wa period
kama ni 26 enter 26 and so on then itakupa ur most fertile day whento have sex..
Hope this will help for those people who are trying to get pregnant

Anonymous said...

Mimi nataka kujua kalenda ya mezani unaweza kutumia inafaa? pili nimebleed tarehe 9/10/2009 je siku nzuri za kushika mimba itakua tarehe ngapi naomba nifahamishe

Anonymous said...

You trie to explin about,but they are supposed to consider the time taken for a spurm to stay in.Thank

Unknown said...

Nilikua nauliza hivi eti ukifanya mapenzi siku moja kabla ya kuingia katika siku zako unaweza kupata mimba? Alafu hivi kuna madhara kufanya mapenzi huku msichana akiwa katika siku zake kwa kutumia condoms.

Anonymous said...

tnx kwa kutujuza mimi huw na bleed tarehe 19 na huenda siku sita baada ya hapo nilimaliza siku 6 nikafanya, je naweza kupata mimba?

JUSTINA JAMES said...

Hallo dada kuhusu kuzuia mimba kwa kalenda ni ngumu sana kuelewa na isitoshe kama maelezo si ya mtaalamu husika. Jaribu kutafuta maelezo sahihi kutoka kwa Dr. wa wanawake au SCIENIFIC DETAILS KUTOKA KWA WATAALAMU WA SCIENCE HIYO. SIWEZI SEMA MOJA KWA MOJA KWAMBA HAUPO SAHIHI, ILA KWENYE USHAURI WAKO UNGEWASHAURI WADAU WAWAONE WATAALAMU WAHUSIKA YAANI DR. NA SI WAUGUZI AU WATAALAMU WAKUSIKIA.

Justina S..

Anonymous said...

je unaweza kupata mimba ukifanya mapenzi siku ya kwanza unayoanza period?

Anonymous said...

Mimi huwa natumia kalenda na condoms. Ikiwa siku hatari tunatumia condoms kama tunatakakufanya tendo la ndoa na mume wangu na siku salama huwa hatutumii condom kwa raha zetu. Jinsi tunavyohesabu nikianza siku zangu tunaanza kuhesabu siku kumi toka naanza period baaada ya siku kumi hatutumii condom tunahesabu tena siku kumi ndo salama baada ya hapo tunasubiri tena nianze siku zangu. Siku za mzunguko wangu ni 26 mpaka 28. Kama sijafahamika siku 10 toka naanza period salama siku 10 zinazofuata si salama halafu siku 10 zinazofuate ni salama mpaka pale natopata tena siku zangu.

Abuu jamaal said...

mimi ni mgeni wa safu hii ila nimeelimika kupitia safu hii sasa nauliza hivi nimesikia kuwa mtu kama anashirikiana na mke wako kila siku hawezi kushika mimba kwasababu mbegu za mwanaume siyo nyingi kauli hii ni kweli au ni uzushi?

Abuu jamaal said...

nauliza kuwa eti mke na mume kama wanashirikiana tendo la ndoa kila siku hapati mimba nimesikia hivyo ni kweli au ni uzushi?

Anonymous said...

je kwa wenye mzunguko wa siku 30 je ni siku gani za kupata ujauzito maanna hapo nimeona umezungumzia wenye siku 28