Friday, September 4, 2009

Dawa ya malaria kwa watoto yenye ladha ya Cherry


Dawa mpya ya malaria imetengenezwa na kuanza kuuzwa madukani yenye ladha ya cherry, lengo lake likiwa ni kuwafanya watoto wakubali kunywa dawa hiyo kwa urahisi. Tunajua dawa nyingi za vidonge za malaria ni chungu, suala ambalo linaleta kizuizi katika kutibiwa vizuri watoto wanaopatwa na malaria.

Watoto wengi hukataa kula dawa hizo hata baada ya kuongezwa sukari. Lakini dawa tamu inayopendwa na watoto ya malaria iitwayo Coartem inaonekana kuwa suluhisho la tatizo hilo.

Dawa hiyo huweza kuyeyuka katika maji na maziwa ya mama, lakini hunukia kama juice ya matunda ya cherry!.
Inatarajiwa kuwa dawa hiyo itaanza kutumika katika nchi za Kiafrika hivi karibuni.

Kumbuka kuwa:
Ugonjwa wa Malaria ni ugonjwa unaoua zaidi duniani, ambapo watu milioni 1 kufariki dunia kila mwaka kutokakana na ugonjwa huo. Wahanga wakubwa wa ugonjwa wa malaria ni watoto.

1 comments:

Anonymous said...

Pole na kazi dada kwa kutuelimisha vijana wenzio. Mimi ninatatizo moja nilizaa mtoto 1 nikaja nikashika mimba ikatoka. Lakini mpka sasa natafuta mtoto sipati je nifanyeje? na tarehe zangu hubadilika kila mwezi.