Thursday, August 6, 2009

Wanawake kiini cha watoto kupata mtindio wa ubongo


Wastani wa asilimia mbili ya watoto wanaozaliwa nchi huwa na tatizo la mtindio wa ubongo kutokana na mama zao kutofanya mazoezi wakati wa ujauzito.

Mbali ya maelfu ya watoto wengine ambao hufariki wakati wa kuzaliwa wengine wengi hupata ulemavu wa kudumu kutokana na wauguzi kulazimika kunyofoa baadhi ya viungo vyao wakati wa kuwasaidia mama zao kujifungua.

Hayo yalibainishwa jana na mtaalam wa mazoezi ya viungo kutoka katika hospitali ya Aga khan ya jijini Dsm, Dk Gilberi Kigadye alipokuwa akizungumzia umuhimu wa wanawake wajawazito kufanya mazoezi kabla na baada ya kujifungua.

Alisema matatizo hayo husabishwa na mama mjamzito kutofanya mazoezi na hivyo kushindwa kusukuma mtoto ipaswavyo wakati wa kujifungua.

"Wakina mama wasiofanya mazoezi wakati wa kujifungua huwa hawana nguvu ya kumsukuma mtoto, kama wakati wa mtoto kutoka utakuwa umefika mama akishindwa kumsukuma huyo mtoto atakunywa maji machafu halafu pindi akitoka akiivuta hewa lazima itamuathiri akili na hivyo kuwa na mtindio wa ubongo," alisema Kigadye:

"Wakati mwingine utakuta mtoto anatanguliza mkono, kama huyo mtoto atapona unaweza kumkuta akiwa na kilema cha mkono kutokana na kuvutwa,"

Kigadye aliyekuwa akizungumzia katika chumba maalum cha mazoezi cha hospitali hiyo alisema, ni vyema wakinamama wajawazito wakapata ushauri wa kitaalam juu ya namna ya kufanya mazoezi na aina ya mazoezi wanayotakiwa kufanya ili yawasaidie wakati wa kujifungua.

"Hapa Aga Khan tuna hiki kitengo cha mazoezi kwa ajili ya akina mama wajawazito na wagonjwa wanaotakiwa kufanya mazoezi ya viungo ni vyema mama mjamzito akapata ushauri wa mtaalam kabla ya kufanya mazoezi, katika hiki kitengo pia tunatoa ushauru huo," alisema Kigadye.

Alisema pia kuwa asilimia kubwa ya wanawake hupata matatizo ya mgongo miezi sita baada ya kujifungua kutokana na kutofanya mazoezi baada ya kujifungua.

Na Fredy Azzah

0 comments: