Saturday, August 22, 2009

Kutokwa na UCHAFU UKENI!



 Hakika mapenzi ni matamu hakuna asiyelifahamu hili na mapenzi kwa kawaida hushirikisha vishiriki ngono kama kupapasana, kubusiana na hata mambo fulani ya kula koni na kuzama chumvini. Hakika uke ni sehemu muhimu sana ya mwanamke inayoweza kuamsha hisia za mwanamme wake ama kuzipoteza,kumthaminisha ama kumshusha dhamani endapo mwanamke atashindwa kujiweka katika hali ya usafi ama kukabiliana na matatizo ya kutokwa na uchafu ukeni. Hivyop kwa kutambua hili leo nimeamua kuandika mada hii ili kuwasaidia wale wote wenye tatizo kama hili.....

Kimsingi wanawake wote hutokwa na uchafu kidogo ukeni ambao ni mweusi kama maji, maziwa au njano ambao humfanya ama awashe au atowe harufu mbaya pale anaposhindwa kukabiriana na hali ya usafi wake. Hata hivyo, wanawake wengi kipindi cha ujauzito hukumbwa na hali hii mara kwa mara na huwashwa. Uchafu husababishwa na mambo mbalimbali ambapo mengi husumbua japo si hatari. Zifuatazo ni aina za uchafu ambao wengi huwakumba na jinsi unavyoweza kukabiriana na tatizo hilo.

Uchafu wa majimaji wenye rangi mchanganyiko wa kijani na njano au nyeupe.
Mwanamke aliyena tatizo la kutokwa na aina hii ya uchafu hujikuta ananuka na kujikuna sehemu zake za siri, na huu unawezekanai kuwa ni ugongwa wa Trichomos kwani pindi anaposikia haja ndogo hujisikia kuchomwa sana na maumivu ambapo wakati mwingine hujikuta anavimba.

Uchafu wa aina hii huonekana kama picha kushoto inavyoonyesha hivyo mwanamke ambaye atakumbwa na tatizo kama hili ni rahisi kumfanya mpenzi wake apoteze hamu ya kushiriki naye tendo la ndoa na kama ni mpenzi basi huweza kujikuta kila kukicha anashindwa kudumu na mwanaume kwani hukimbiwa kutokana na kushindwa kwao kukabiriana na tatizo hilo.

Endapo una tatizo hili ni muhimu sana kuhakikisha unaweka viungo vya uke wako katika hali ya usafi wa kutosha, na ni vema unaposafisha uke wako uhakikishe unatumia majiya uvuguvugu pamoja na siki au maji la limao yaliyochanganywa na maji ambapo unapaswa kutumia vijiko 3 vya siki kwenye maji lita moja yaliyochemshwa. Ni muhimu mgojwa asafishe uke wake mara moja hadi tatu kila siku mpaka apone!

Hata hivyio endapo tatizo hilo linakuwa kubwa, mgonjwa anapaswa kutumia dawa za kuchomeka ukeni ambazo zina metronidazole au dawa zingine zinazoshauriwa na trichomonas. Ikiwa hali mbaya sana anapaswa kumeza metronidazole kwa kiasi cha gram mbili [meza kwa mpigo].

Aidha, inawezekana kuwa mwanaume ana ugonjwa pia wa trichomonas ingawa hajisikii hali ya kuumwa hata kidogo hivyo endaapo mwanamke atarudiwa na ugonjwa huu mara baad a ya kujitibu basi anapaswa kurudia kumeza gram mbili za metronidazole, lakini ni kama ugonjwa huo mkubwa.

Uchafu ambao uko kama jibini au siagi na unanuka kama uyoga au mkate.
Hali hii inapojitokeza kwa mwanamke hujikuta anawashwa sana ukeni na midomo ya uke huwa na rangi nyekundu na huuma sana ambapo pindi mhusika napotaka kukojoa husikia maumivu makali sana. Hali hii huwakumba sana wanawake wajawazito pamoja na wale wenye ugonjwa wa kisukari, wale waliokuwa wakitumia antibiotics au vidonge vya kuzuia ujauzito.

Endapo una tatizo hili ni muhimu sana kuhakikisha unaweka viungo vya uke wako katika hali ya usafi wa kutosha, na ni vema unaposafisha uke wako uhakikishe unatumia maji pamoja na sikiau GV vijiko viwili kwa nusu lita au kutumia vidonge viwili vya nystatin vya kuchomeka ukeni au dawa nyingine ya thrush kama siyo kuweka maziwa mgando yaliyochachuka kwenye uke husemakana ni dawa nzuri ya kienyeji inayotibu tatizo hili.

By Mwakilanga

ITAENDELEA.....

4 comments:

Anonymous said...

Mwakilanga hongera sana kwa makala hii elimishaji na kweli kwamba akina mama na dada zetu wanashauri kwenda kuwaona madaktari wa magonjwa ya kina mama kupimwa na kutumia vidonge vya kusafisha vijia vyao vya uzazi.

Ajabu na kweli kwamba wengi hawajui hata kama dawa hizo zipo. Kumbe nawashauri tu wakapate dawa hizo za kuzuia mrundikano wa bacteria wabaya wanaoweza kusababisha madhara ndani ya kiungo hiki muhimu kipendwacho na wote wale wenye mikia.
Hata hivyo umefanya vizuri sana kuitoa makala hii ili wale wanaopenda kuzamisha midomo yao chumvini tunduni...basi wakome. Ni hatari sana haswa zama hizi za UKIMWI na maambukizo ya fungus ambazo hupenda kukaa humu kwa wale walioadhirika..ndo maana ni vizuri kufanya matayarisho ya mapenzi bila kugusa kwa mdomo eneo hilo ni hatari...hata yule jamaa yetu mzee fimbo cheza..hulalamika sana matundu mengine akiingia..yanatisha kama haya...ndo maana tumieni mishaa au taa wakati wa tendo la kupigishana gwaride..ili mtu unaweza kuona kule tunduni kukoja kwa nje..maana dalili hizi huja kwa juu juu pia.

Asante sana kwa yote.
Nikutakia maisha mema endeleza kazi hii na mdau na msomaji mwenzagu..tubadilike..maisha ya kula chumvi..tutamiza na pilau ya chumvi kama hizo hapo juu..

mdau..

Anonymous said...

Hongera sana uliye anzisha mada hii yaani umelenga pale penyewe panapo takiwa, umewagusa sasa vijana wakiwemo na wale wanaojiita wazee vijana. Ni kweli kabisa tatizo hili la kutokwa na uchafu ukeni huwakumba sana kinamama/kinadada.

Kwani unakuta mwananmke mwingine hajijui kama anahilo hilo tatizo, inafika kipindi linakuwa sugu. Na vijana wengi hupenda sana kurahisisha mambo kwa kujiachia kama hivyo mtu kuingia chumvini na matokeo yake wengi hupata fangasi za mdomoni na huanza kujiuliza ni wapi alikopatia kumbe ni kule chumvini alikoingia. Na hii nihatari sana kuambukizwa magonjwa mbalimbali yakiwemo hayo ya fangas, Ukimwi na mengineyo.

Yatupasa tuwe na matayarisho pindi mtu/watu watakapo takafanya tendo la ndoa bila kugusa na mdomo uke wa mwanamke.

Na wengine bila kulabwa ukeni hawasikii raha ya lendo la ndoa na inasemekana wengine ndiko stimu zinakopanda.

Ninachoshauri ni kwamba pindi ufanyapo tendo la ndoa yakupasa usizime taa kwani kile kitendo cha ww kuzima taa unajikuta waingia chumvini bila kujua huko kwenye uke kukoje kukoje, so tuwe makini sana hususani vijana wa sasa na hao wanaojiita wazee vijana.

Jacky

Anonymous said...

Nimekusoma nimekuelewa sana kwa mada yako nzuri yenye kuelimisha.
Hili ni tatizo sugu sana hasa kwa wakina mama na wasichana, hii inatokana mara nyingi na maambukizi ya magonjwa ya Zinaa STDs au wakati hutokana na maumbile ,vilile pia hutokana na uchafu wa mtu mwenyewe akiwa hajiweki sawa kila mara..

Sasa hii inakuwa kero zaidi pale inapofikia swala mambo flani ya mapenzi kutomasana, kulambana, kunyinyana kila kona mwili tatizo hili huwa kero na inaweza hata kupoteza kabisa shuku ya kuduu mapenzi labda ni kutokana na harufu kali, au utando utando mweupe utakaonekana wakati jamaa akiwa anaenda chumvini...
Nimalizie kwa kushauri tu tuwe makini katika kujiangalia usafi wa miili yetu wakati tunaenda KU DUU... Hakikisha upo powa jikague kila idara ili usije kuwa kero kwa mwenzako...

007

Anonymous said...

Mhh nashukuru kwa kupitia hii blog maana natafuta kweli dawa kwaajili ya hilo tatizo maana hata nimesoma nimeona umeandika dawa nyingi so sifahamu ipi na ipi ndio itakayo faa kutoa hiyo harufu chafu ukeni mimi nimeshaenda kila hospt ila mafanikio hakuna na kila dawa nimeshameza sasa sijui napaswa kutumia ipi kati ya hizi ulizozitaja hapo juu nashukuru kama nitapata jibu hili maana nimeona umetoa na dawa za kutumia na nimeenda ulizia maduka ya dawa wanasema hawana hizo dawa naomba msaada wajameni