Tuesday, August 25, 2009

KUTOKWA NA UCHAFU UKENI PART II


Uchafu mzito ulio kama maziwa na wenye harufu mbaya
Huu unawezekana kuwa ugonjwa [uke huwa kama picha inavyoonyesha]unaosababishwa na chembechembe ambazo huitwa haemophilus. Uchunguzi maalum unahitajika ili kupambanua ugonjwa huu na trichomonas. Safisha uke kwa siki na maji kama nilivyosema katika sehemu ya kwanza ya mada hii, lakini unapaswa pia kutumia vidonge vyakuchomeka kwenye uke vya sulphathiazole mara mbili kutwa kwa wiki 2.


Ugonjwa huu unapompata mwanamke kwanza kabisa hukosa amani hata ya kukutana na mwenza wake na hasa kama mwenza huyo ni mtundu katika mambo fulani ya vishirikishi ngono yaani halianzishi hadi apime oil na kuzama chumvini. Hivyo mwanamke yoyote mwenye tatizo hili ni vema asilipuuziye kwa kuamua kushiriki tendo bila kupata tiba hata kama utajisafi vipi.

Uchafu wa majimaji mweusi au rangi ya kijivujivu ambao una damu na harufu mbaya
Mwanamke mwenye ugonjwa huu huwa amefikia hatua mbaya zaidi kwani yawezekana tayari kansa ikawa imeshamtafuna katika maumbile yake ya uke. Hata hivyo kansa sehemu za uke mara nyingi huwapata wanawake walio na umri zaidi ya miaka 40, na dalili ya kwanza inaweza kuwa ni upungufu wa damu mwilini au kutumia hedhi isiyo ya kawaida na kujisikia uzito au kuona uvimbe wenye maumivu katika kinena [kama una hali hii nenda kamuone daktari haraka].

Ugonjwa huu pia huambatani ambapo mtu akipatwa na homa anaweza nkunjwa dawa za kuua vijidudu au kumuona dk.

KIMSINGI: mwanamke yoyote yule ambaye anasumbuliwa na uchafu wa muda mrefu na hata akiutibu haupunguwei licha ya kufanya matibabu ya awali kama nilivyobaibisha hapo juu anapaswa kwenda kumuona daktari.

MUHIMU!

Mwanamke yoyote yule anaweza kuepuka magonjwa mengi ya ukeni endapo atafanya haya yafuatayo:-

Kuweka viungo vya uke wake katika hali ya usafi.
Mwanamke wakati anaogo anatakiwa kuhakikisha anasafisha vema uke wake kwa kutumia maji na sabubi na si kupuuzia kwa kujipapasa tu maana kuna wengine hujifanya kuona kinyaa yaani ataoga kote kisha huko anapanguza na toilet pepar kisha biashara imeisha hii ni mbaya, hivyo hata kama ukiwa kwenye baridi ama ukame wa maji hakikisha hulali bila kusafisha uke wako!

Kojoa baada ya kukutana na mwanaume
Hii ni kwa wale ndugu zangu wanaokwenda uwanja wa taifa kucheza mechi na kushuka dimbani pasipo kuwa na jezi yaani wao ni peku peku sasa wengine wakimalzia tu mechi huinuka kisha kujifuta na toilet paper na kujisafisha kidogo kisha hao wanakamata chupi na kuvaa huku akisindikiza na katoilet peapr chini yaani anaiweka kama vile awekavyo pedi, sasa hii ni hatari kwa majongwa kama niliyoyaeleza kwenye mada zangu.

Hakikisha umejipangusa au kujitawaza vizuri baada ya kwenda choo.
Mwanamke naamini anajua jinsi ya kujisafisha kwani zoezi hili hufundishwa tangu wakiwa wadogo lakini kama haujui ni vema ukajiswafi yaani kujipangusa kutoka mbele kwenda nyuma kwani kujipangusa kwa kwenda mbele husababisha mikroba, ameba au minyoo kwenye uke.

7 comments:

Anonymous said...

dah!

kuna wanawake wengine ukimnanihii ananuka kama kafa sasa najiuliza akifa atanukaje?- Robert

Anonymous said...

Somo zuri sana, toa mafundisho zaidi juu y usafi wa wanawake na wasichana pia. Dos na Donts tafadhali ili waonekane warembo.
Maana wengine wanatisha unamuona nje anameremeta lakini ukifika katika utamu wake utafikiri hapana mwenyewe.
By Mumeo

Anonymous said...

Msaada,
kwa yeyote mwenye idea nina msichana wangu wa ndani ana tatizo ikifika siku zake huwa damu ina toka ya kijivu yenye ute ute wa kuvutika nilimpeleka hospitali bila msaada ila walisema ni hali ya kawaida je nikweli kwani sasa ni muda tangu hiyo hali ianze mwenye maoni tofauti?

Anonymous said...

Greetings

It is my first time here. I just wanted to say hi!

Anonymous said...

Nimepita huku leo nimekuta mambo mazuri sana, sitaacha kupita.

nisaidie, mbona mimi sina ule ute laini katika uke wangu? hii ni wiki ya pili sasa.
nilipatwa na hali ya ute ute wakati wa tarehe za mwisho za mwezi uliopita, ilikuwa karibu na period, then sikupata hedhi zangu, matokeo yake sasa ule ute umepotea kabisa, uke wangu ni mkavu sana hata sina amani jamani.
nilipata kukutana na mpenzi wangu mara mbili, au nimenasa? wow! nitashukuru sana

Unknown said...

Sasaa dada,mimi nashindwa kujielewa,somo lako nimelielewa vizuri Mungu akubariki,lakini mm tatizo langu ni wakati mwingine ute wangu unatoka na vijidamu,ule mwepesi na nkikaribia breed kuna uchafu huwa unatoka warangi kama ya kahawiya,ila ute haunuki na wala siwashwi,ni tatizo gani hli dada,alafu hata nikiwa kwny mamboz baada ya nkiwa najisafisha ute huwa na vjidamu au wakati mwingine huwa kama wa cream,nisaidieni ndugu zangu.

Anonymous said...

Greetings,

This is a inquiry for the webmaster/admin here at mashosti.blogspot.com.

Can I use part of the information from your post above if I provide a backlink back to your website?

Thanks,
Alex