Friday, July 31, 2009

Mazoezi magumu kwa shosti mwenye mimba changa ni hatariii


Watafiti nchini Denmark wamesema mazoezi magumu kwa mwanamke mwenye mimba changa yanaweza yakamsababishia mjamzito athari ya mimba kuharibika mara dufu.

Pia watafiti hao wamegundua kwamba kukimbia kwa taratibu yaani jogging, michezo wa mpira na michezo ya kutumia racket yote inachangia hatari ya kuharibika kwa mimba sawa na kufanya mazoezi ya masaa saba kwa wiki.

Hata hivyo serikali ya Denmark inashauri mjamzito kufanya mazoezi kama kanauni ya lazima wakati wote wa kipindi cha ujauzito.

0 comments: