Thursday, January 17, 2008

Jinsi ya kuzuia na kutibu Kuharisha wakati unapokuwa safarini

Jinsi ya kuzuia na kutibu Kuharisha wakati unapokuwa safarini

Kwa nini niharishe wakati ninasafiri?
Kuna maambukizo mengi watu hupata wakati wanaposafiri na ambayo huleta kuharisha. Mengi ya haya maambukizo hayadhuru watu wanaoishi katika sehemu hizo ambazo wewe unasafiri kwani wao huenda walishaugua kabla (na sasa wamejenga kinga). Watu pia huharisha wakati wanaposafiri kutokana na uchovu wa safari na kubadilisha chakula.

Nitajuaje kama kuharisha kwangu ni maambukizo au ni kutokana na sababu nyingine?
Ni vigumu kusema tofauti yake. Kama unaenda choo laini 2-3 kwa kutwa na bila dalili nyingine zozote, kuharisha kwako sana sana huenda haukuambukizwa na vimelea vibaya. Maambukizi haya yatafuatwa na kupata choo cha maji maji mara nyingi. Dalili nyingine ni pamoja na kuharisha damu, homa, maumivu ya tumbo na kichefu chefu.

Nitazuiaje kuharisha?
Kitu cha maana kabisa na rahisi ili kuzuia kuharisha ni kuosha mikono mara kwa mara. Kufanya hivi ni muhimu sana haswa kabla ya kula chakula, pia mara nyingi kuosha mikono mara kwa mara ni vizuri. Kwa kuwa sabuni na maji sio ghali na hupatikana kila mara, kuna vitambaa vilivyolowekwa katika dawa za kuulia wadudu (hufanya kazi vizuri sana) huwa ni rahisi zaidi kutumia wakati ambapo sabuni na maji havikupatikana. Vitambaa hivi hupatikana katika maduka mengi ya dawa, hata ya vyakula au stoo za vitu mchanganyiko huko Umarekani, vichukue vitambaa hivi uendapo safari. Kama hujui jinsi ya kuvipata, mwulize daktari au muuguzi wako.

Vyakula vingine ni salama zaidi. Chakula chochote au kinywaji ambacho kina moto sana wakati kinapoandaliwa ni salama. Mikate, pipi pia ni salama. Vyakula ambavyo vina hatari ya kuleta madhara na kukufanya uwe mgonjwani kama mboga mboga mbichi, saladi na vinginevyo vibichi au vilivyopikwa na kuiva nusu kama vile samaki na nyama. Kama utaosha mikono yako na kutumia kisu kisafi kumenya na kukata tunda, kwa kawaida ni salama. Epuka matunda ambayo hayana kumenywa kama vile matunda damu. Vyakula vya maziwa kama vile maziwa na jibini si salama labda kama vimesindikwa kwa ufundi (kuchemsha kwa mvuke). Unaweza kutengeneza maziwa salama kwa kuyachemsha mpaka kuchemka na kuyaacha yapoe. Maziwa ya pakiti (irradiated milk) ni salama kwa kunywa.

Maji yanaweza kukufanya ukawa mgonjwa pia. Kama maziwa, ukichemsha maji yako yatakuwa safi na salama kwa kunya. Maji yauzwayo, yaliyohifadhiwa kwenye chupa pia kwa kawaida ni salama kwa kunywa. Vinywaji vilivyosindikwa kwenye chupa (vyenye kutoa vipele vya hewa kama vile soda) pia ni salama kwa kunywa. Hewa ya carbon inayotiwa katika vinywaji vilivyosindikwa pia huua vimelea kwa kipindi cha masaa manne, hata hivyo kutia hewa hii katika bomba la maji haifanyi maji yake kuwa salama kunywa kwani maji yaliyochanganywa hayakuwa yamechemshwa. Ni lazima uepuke kutumia vibonge vya barafu labda viwe vimetengenezwa na maji safi na pia wakati wa kupiga mswaki utumie maji safi na salama.

Itakusaidia zaidi endapo utafanikiwa kuepuka vyakula vya aina fulani kwa kuwa tumbo lako halikuvizoea japo vilizoeleka zamani.

Nifanye nini kama nitaharisha?
Kuna aina mbili za dawa za kuzuia kuharisha kwa wasafiri. Ya kwanza ni zile dawa za kupunguza kasi ya kuharisha lakini hazitibu maambukizo yaliyoleta kuharisha. Dawa hizi zinasaidia kupunguza dalili za ugonjwa. Dawa zinazotumika sana zinaitwa loperamide (“Imodium”) na Bismuth subsalicylate (“Pepto-bismol”), amabzo zote zinapatikana maduka yote ya dawa bila ya agizo la daktari. Dawa hizi zisitumiwe na watoto wadogo.

Pia, kuna (antibiotics) dawa zinazoua vimelea vibaya ndipo hutibu ugonjwa. Kwa kuzitumia dawa hizi huweza kupunguza idadi ya siku za ugonjwa.

Wakati unapoharisha maji maji ni lazima utumie (antibiotic) dawa za kuulia vimelea vya ugonjwa ambazo daktari au muuguzi wako atakupa uchukue safarini. Unaweza pia kutumia loperamidend Bismuth subsalicylate kuzia kuharisha mpaka dawa ya kuulia vimelea vibaya ifanye kazi. Kama uko
taabani, una homa au unaona damu katika choo chako, ni lazima utumie dawa ya kuulia vimelea (antibiotic) na SIO ile ya leperamide au Bismuth subsalicylate.


Vitu vya kukumbuka wakati wa kusafiri (Kuchukua pamoja na karatasi za safari)

Usipatwe na Kuharisha

OSHA MIKONO, huwezi kuosha mikono vya kutosha, haswa kabla ya kula (tumia vile vitambaa vilivyowekwa dawa ya kuulia vimelea vibaya kama Purell au Aavanguard kama ni rahisi zaidi kutumia)

Epuka vyakula hivi:
Vibichi, au nyama, samaki isivyoiva vizuri, maziwa ambayo hayajachemshwa au jibini, majani ya mboga mboga. Matunda ni lazima yaandaliwe kwa njia ya usafi.

Maji na Maziwa
Vinaweza kufanywa kuwa safi na salama kunywa kwa kuchemsha na kuacha chini yapoe. Maji yanayouzwa katika chupa kwa kawaida ni salama.

Kama umeenda choo laini mara moja au mbili kwa siku tumia dawa ya kukusaidia katika dalili hizi, lakini choo cha maji maji kabisa haswa kuchanganyika na damu, maumivu na homa, tumia dawa ile ya kuulia vimelea vibaya (antibiotic).
DAWA ZA KUZUIA KUHARISHA

Wakati uonapo dalili:

Loperamide (“Imodium”)
Matumizi:
Kunywa vidonge viwili kwa kuanzia, kisha kunywa kidonge kimoja kila upatapo choo (usinywe zaidi ya 8 katika masaa 24). Usiwape watoto wachanga, wadogo au ukiwa mja mzito.

Bismuth subsalicylate (“Pepto-bismol”)
Matumizi:
Kama ni vidonge meza vidonge viwili kila baada ya dakika 30 mpaka kuharisha kupungue. Hata hivyo usinywe vidonge zaidi ya 16 katika masaa 24. Kama unakunywa vitu vya maji maji,

kunywa vijiko vya chai 6 (30 mls) kila baada ya dakika 30 mpaka kuharisha kupungue. Usinywe vidonge zaidi ya 8 katika masaa 24. Usiwape watoto wachanga na watoto wadogo.

Kutibu Maambukizo

Antibiotic:
Daktari au muuguzi wako atakupa dawa ya antibiotic kusafiri nayo unywe ukipatwa na kuharisha kubaya. Hakikisha kuwa unaelewa jinsi ya kunywa dawa hizi kabla ya kuondoka katika ofisi ya daktari au muuguzi. Majina ya dawa za antibiotic zinazotumika na kujulikana sana ni kama Azithromycin (Zithromax), Ciproflaxacin, Levofloxacin (Levoquin) na Fifaxaamin.

0 comments: