Friday, May 25, 2001

JINSI YA KUTOA MIMBA KWA KUTUMIA VIDONGE VYA MISOPROSTOL




Yafuatayo ni maelekezo kuhusu matumizi ya vidonge vya Misoprostol (vidonge hivi hupatikana kwa majina ya Misotac, Citotec au Kontrac):

* Tahadhari za kuchukua
* Jinsi gani vidonge hivi vinatumika
* Vipimo bora vya dawa na matumizi yake
* Matokeo gani wanawake watarajie
* Madhara/matatizo yanayoweza kujitokeza


Kutumia vidonge vya Misoprostol (Misotec, Cytotec au Kontrac) peke yake hufanikiwa kutoa mimba kwa asilimia 80 hadi 90. Taarifa hii inatokana na utafiti uliofanywa na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO).


Baadhi ya wanawake hujaribu kutoa mimba kwa kuingiza vifaa vyenye ncha kali au vitu vichafu tumboni au kwa kujipiga makonde tumboni. Vitendo hivi ni hatarishi na kamwe mwanamke yeyote asifanye hivyo, kwa kuwa vinaweza kusababisha majeraha yenye athari kubwa tumboni, ikiwa pamoja na kuvuja damu nyingi na hivyo kuleta kifo.

Maamuzi ya kutoa mimba ni jambo gumu sana kwa wanawake walio wengi. Iwapo huwezi kumweleza muhudumu wako wa afya kuhusu kutoa mimba au njia nyinginezo, tunashauri ujadili suala hilo na rafiki unayemwamini au ndugu wa karibu. Haswa tunashauri binti au wasichana kuongea na wazazi /mzazi wao/wake au mtu mzima anayemwamini kuhusu hali yake, uamuzi alionao na jinsi ya kutekeleza utoaji mimba.

Iwapo mwanamke yeyote anadhamira ya dhati ya kukatiza mimba yake na hana njia nyingine ya kumwezesha kufanya hivyo, ni vyema asome kwanza maelekezo haya kwa makini.

Ni vyema pia iwapo atayajadili na mmoja kati ya marafiki zake. Wala usijaribu kutekeleza jambo hili peke yako.

JINSI YA KUTOA MIMBA KWA KUTUMIA MISOPROSTOL na TAADHARI ZA KUCHUA




Mwanamke yeyote asijaribu kutoa mimba peke yake iwapo ana mimba inayozidi wiki 12, ni lazima amuombe rafiki yake awe pamoja naye. Shirika la Afya Ulimwenguni linaruhusu matumizi ya dawa ya Misoprostol nyumbani hadi wiki ya 9 ya ujauzito.

Kati ya wiki ya 9 na 12 uwezekano wa matatizo kutokeza unaongezeka na mwanamke anapashwa kuchukua tahadhari zaidi. Ushauri wa jinsi ya kutumia Misoprostol ni ule ule kwa wiki 12 za kwanza za ujauzito.

Vidonge vya Misoprostol husababisha maumivu ya tumbo. Matokeo yake ni kizazi kujaribu kutoa nje ujauzito. Mwanamke anaweza kupatwa na maumivu makali ya tumbo, kutokwa na damu kwenye uke inayozidi ile ya hedhi ya kawaida, kichefuchefu, kutapika na/au kuharisha.

Kuna uwezekano wa damu kuvuja kwa wingi, hali amabayo inambidi mwanamke ahudumiwe na dakatari. Misoprostol hufanikiwa kutoa mimba kwa zaidi ya asilimia 80%. Vidonge hivi vinapatikana katika maduka ya dawa za binadamu (pharmacy) karibu nchi zote ulimwenguni.

Hali na matokeo ya kutoaji mimba kwa kutumia Misoprostol yanafanana na yale ya mimba poromoka (yenyewe). Iwapo kutakuwa na tatizo, mwanamke anatakiwa kwenda kwenye kituo cha afya na anaweza kumueleza daktari au muhudumu kuwa mimba yake imeporomoka.

Jinsi ya kutibu hali hiyo pia inafanana na ile ya mimba iliyoporomoka. Iwapo pia kumejitokeza tatizo mwanamke anaweza kwenda kituo cha afya na kumweleza daktari au muhudumu kuwa mimba yake imeporomoka. Dakatari au muhudumu wa afya atamtibu kana kwamba ameharibikiwa na mimba. Hakuna njia yoyote ya kumwezesha daktari kugundua kuwa mwanamke ametumia dawa hii ya Misoprostol.

Yafuatayo ni maelezo muhimu ambayo mwanamke yeyote anayetaka kutoa mimba kwa kutumia dawa hizi anapashwa kufahamu:



Mwanamke awe na uhakika kuwa anaujauzito


Anaweza kuchukua kipimo cha ujauzito au kupita kwenye ultrasound. Kipimo cha ultrasound kitaonyesha iwapo mwanamke ana mimba na umri wa mimba hiyo. Wanawake walio wengi hujitambua kuwa na mimba pindi wanapojiisi kuwa wenye kuhitaji sana ngono na iwapo wamechelea kipindi cha hedhi. kichefuchefu, matiti kuvimba na uchovu ni miongoni mwa dalili za mwanzo za ujauzito.


Misoprostol inapashwa kutumika iwapo mwanamke ana uhakika wa asilimia 100% kuwa anataka kutoa mimba.



Mwanamke asitumie Misoprostol baada ya mimba kufikia wiki 12 na zaidi

Mimba inatimiza wiki 9 kwa maana ya siku 63 (au wiki 12) tukihesabu kuanzia siku ya kwanza ya hedhi ya mwisho. Mwanamke anawezahesabu kwa usahihi siku zake za ujauzito. Ili kufanya hivyo ni lazima akumbuke tarehe ya kuanza kwa hedhi yake ya mwisho, ataanza kuhesabu siku hiyo hadi siku aliyofikia kwa sasa. Iwapo mwanamke anafikiri amekuwa na ujauzito kwa zaidi ya wiki 12, au iwapo kipimo cha ultrasound kitaonyesha hivyo, hatumshauri kumeza vidonge vya Misoprostol isipokuwa chini ya uangalizi wa daktari. Hata hivyo, dawa hii inawezafanya kazi ila uwezekano wa kutokwa na damu kwa wingi, kupatwa na maumivu makali na athari zingine zaweza jitokeza katika mimba za baadaye.


Mwanamke asijaribu kamwe kutoa mimba akiwa peke yake

Unapotoa mimba ni muhimu sana kuwa na mtu karibu, ambaye aweza kuwa mwenzi wako (mme), rafiki au ndugu wa karibu ambaye anafahamu nini unatekeleza na ataweza kusaidia iwapo yatajitokeza matatizo yoyote. Atakapoanza kutokwa na damu, ni vyema awepo mtu wa kusaidia pindi hali itamzidia.


Dawa ya Misoprostol itumiwe bila usimamizi wa muhudumu wa afya iwapo tu mwanamke hana ugonjwa wowote wa hatari

Magonjwa mengi hayahatarishi utoaji mimba. Hata hivyo baadhi ya magonjwa kama vile anaemia (kupungukiwa damu), unaweza sababisha damu nyingi sana kupotea.



Epuka matumizi ya madawa ya kulevya na pombe (kileo) wakati unatumia Misoprostol

Inabidi mwanamke ajitambue na kujidhibiti wakati huu. Anaweza kunywa na kula kama kawaida, isipokuwa tu kutokana na kusikia kichefuchefu tunashauri ale kidogo tu.





Misoprostol itumiwe tu iwapo usafiri wa kumwezesha mwanamke kufika hospitali haraka unapatikana

Kwa jinsi hiyo itakuwa rahisi kumpa huduma ya matibabu iwapo kutakuwa na matatizo.
Misoprostol isitumiwe iwapo kuna uwezekano wa mimba ya nje ya kizazi, hali ambayo hutokea kwa asilimia 1 tu ya mimba zote.

ya mimba inayoitwa ectopic huwa nje ya mji wa uzazi. Mimba hii inaweza kugunduliwa kwa kuchukua kipimo cha ultrasound. Hali hiyo inahitaji matibabu ya daktari wa uzazi au gynecologist ili kufuatilia hali ya mama. Kama hali hii haikutibiwa, kuna uwezekano mkubwa wa kuvuja damu kwa ndani kutokana na mirija ya uzazi kupasuka. Madaktari katika nchi zote ulimwenguni hutibu wanawake wenye matatizo haya, hata kama katika nchi hizo utoaji mimba umeharamishwa. Mimba ya nje ya kizazi haiwezi kutibiwa kwa Misoprostol.
Usitumie Misoprostol iwapo una kipandikizi cha kuzuia mimba (IUD) ukeni.

Kipandikizi hiki ni kijiti kidogo chenye urefu wa ncha tatu (3) hivi ambacho huingizwa ukeni ili kuzuia mimba. Iwapo mwanamke ana kipandikizi na ni mjamzito, ni lazima apime ultrasound kwa sababu uwezekano wa mimba kutunga nje ya mji wa uzazi ni mkubwa. Iwapo mimba imetunga ndani ya mji wa uzazi, ni lazima kuondoa IUD kabla ya kutumia dawa za kutoa mimba.
Kama mwanamke ana mzio wa Misoprostol au homoni yoyote ya prostaglandin (kama dawa aina hizi humletea madhara ya baadaaye), asitumie kabisa dawa hii.

Hali hii hutokea mara chache sana, na mwanamke ataifahamu kama alikwishaitumia siku za nyuma na madhara fulani yakamtokea. Kama hajawahi kutumia dawa hii kabla basi hafahamu kama ana mzio nayo.
Upo uwezekano wa jaribio la kuondoa mimba kwa kutumia Misoprostol kushindwa na mwanamke anapashwa afahamu hivyo.

Uwezekano wa Misoprostol kufanikisha kuondoa mimba ni asilimia 80 – 90% (hii inamaanisha kuwa kati ya mwanamke 1 hadi 2 kati ya kila wanawake 10 hawatafanikisha kutoa mimba zao). Kushindwa hutokea iwapo vidonge havikusababisha damu kuvuja au damu zilivuja lakini mimba ilibaki. Katika hali hii, mwanamke anaweza jaribu tena baada ya siku chache, ila ni lazima achukue kipimo cha ujauzito iwapo hakufanya hivyo kabla ya kutumia Misoprostol katika hatua ya kwanza. Hata hivyo atambue kuwa dawa inaweza kushindwa kwa mara ya pili tena. Kama dawa itashindwa na mwanamke ana mimba inayozidi wiki 12 sasa, na iwapo hakuna dakari anayeweza kumsaidia, anaweza kwenda nchi nyingine ambako utoaji mimba umehalalishwa au anaweza kuamua kubaki na ujauzito wake.
Kama mwanamke atajishuku kuwa na magonjwa ya zinaa, ni lazima amuone daktari ili atibiwe.

Iwapo kuna uwezekano wa ugonjwa wa zinaa kama vile Kisonono au Kaswende, muone daktari ili upewe tiba rasmi. Hatari ya kupatwa na magonjwa haya ni kubwa iwapo mwanamke amebakwa, lakini hujitokeza pia baada ya kufanya ngono isiyo salama na mwenzi wako au mtu yeyote mwingine. Kutokutibu magonjwa ya zinaa kunaongeza hatari ya kuvimba kwa kizazi na mirija ya uzazi. Hali hii huitwa PID yaani uvimbe wa nyonga au kwa kitaalamu salpingitis au adnexitis.

Mwanamke mwenye UKIMWI anaweza kutumia vidonge vya Misoprostol kwa salama, ila tu anaweza akaathiriwa zaidi na upungufu wa damu au athari nyingine
.



UNAWEZA JE KUPATA DAWA YA MISOPROSTOL?

Baadhi ya maduka ya dawa baridi yanauza Misoprostol. Hapa bongo dawa hii huuzwa kwa jina la Misotac. Nchini Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo inajulikana kwa jina la Cytotec au Kontrac.

Katika baadhi ya maduka dawa hii huuzwa kwa maagizo (cheti) ya daktari, katika maduka mengine cheti hakiitajiki. Iwapo utapata shida kununua dawa hii kwenye duka moja, jaribu lingine, au muombe rafiki yako wa kiume akununulie, huenda ikawa rahisi kwake kuipata. Au pia unaweza jaribu kutafuta daktari atakayekubali kukuandikia dawa hiyo. Mara nyingi watu hupata urahisi katika maduka madogo ya dawa baridi.

Iwapo muuza dawa atauliza kwa nini unanunua dawa hii, unaweza kumueleza kuwa dada au rafiki yako anajifungua na anahitaji vidonge hivi ili kupunguza kuvuja damu nyingi.
Wakati mwingine dawa hupatikana kwa watu binafsi. Ni lazima ujiridhishe kuwa dawa utakayo nunua kwa watu hawa ni Misoprostol na wala si dawa nyingine tofauti.
Mtumiaji anunue kwa uchache vidonge vya Misoprostol (Misotac, Cytotec au Kontrac) 12 vya 200mg.

MISOPROSTOL ITUMIWE VIPI?
Matumizi mabaya ya Misoprostol yanaweza kuathiri afya ya mwanamke!!

Ili uweze kutoa mimba, fanya yafuatayo:

* 1. Weka vidonge 4 vya Misoprostol vya 200mg (ikiwa jumla 800mg) chini ya ulimi.

Usimeze vidonge hadi dakika 30 hivi, ili viweze kuyeyuka kabisa!


* 2. Baada ya masaa matatu (3), weka vidonge vingine 4 vya Misoprostol chini ya ulimi. Usimeze pia vidonge hadi dakika 30 hivi, ili viweze kuyeyuka kabisa.

* 3. Baada ya masaa matatu (3), weka vidonge vingine 4 vya Misoprostol chini ya ulimi kwa mara nyingine. Usimeze vidonge hadi dakika 30 hivi, ili viweze kuyeyuka kabisa. Ufanisi utafikia asilimia 80 – 90%.

Utaratibu huu unafanikisha wanawake 8 hadi 9 kutoa mimba zao.
Baada ya dozi ya kwanza ya Misoprostol mtumiaji atarajie kuvuja damu na maumivu ya tumbo. Kwa kawaida kuvuja damu huanza ndani ya saa nne (4) baada ua kumeza vidonge na wakati mwingine huchelewa zaidi. Kuvuja damu ndio dalili ya kwanza kuwa utoaji mimba umeanza. Hali inapoendelea, uvujaji damu na maumivu ya tumbo huongezeka zaidi. Mara nyingi damu huwa nzito na nyingi kuzidi zile za hedhi ya kawaida na huweza kutokea madonge.

Kadri mimba inavyokuwa kubwa ndivyo maumivu yanavyo kuwa makubwa na damu kuwa nyingi.
Kama kutoka kwa mimba kumekamilika damu hupungua na maumivu pia. Wakati wa mimba kutoka hutambulika kwa damu kuwa nyingi zaidi na nzito na maumivu kuwa makali zaidi.
Kulingana na ukubwa wa mimba, mtu anaweza kuona mfuko mdogo ukiwa umezingwa na nyamanyama. Iwapo mwanamke ana mimba ya kama wiki tano hadi sita hataweza kuona mfuko wowote. Baada ya wiki tisa anaweza kuona mfuko na kijitoto kwenye damu.

Kati ya wiki 9 hadi 12 uwekezano wa kupata matatizo huwa ni mkubwa. Iwapo damu haikuvuja baada ya dozi ya tatu, basi mimba haikutoka na mwanamke anaweza kujaribu tena baada ya siku chache au anaweza kuonana na daktari ambaye atakubali kumpa msaada. Kama mwanamke atapenda kuondoa maumivu anaweza kutumia Paracetamol au Panadol.

* Kuvuja damu baada ya kutoa mimba

Damu huendelea kuvuja kidogo kidogo hadi wiki mbili hivi baada ya mimba kutoka, ila huweza pia kuendelea zaidi au kukata mapema. Hedhi ya kawaida hurudi ndani ya wiki 4 hadi 6 hivi baada ya mimba kutoka.

* Kuhakikisha kama mimba imetoka

Baadhi ya wanawake hutokwa damu bila ya mimba kutoka. Kwa hiyo ni muhimu kujihakikishia kama kweli mimba imetoka. Vipimo vya mimba vya kawaida huchukua wiki 3 hadi 4 kuanza kutoa majibu. Hivyo basi, mwanamke achukue kipimo cha ultrasound baada ya wiki 1 ili kupata uhakika kuwa mimba ilitoka. Kama mimba ilifanikiwa kutoka, dalili za kawaida za ujauzito zitapotea.

* Madhara yatokanayo na matumizi ya dawa:

Madhara ya kawaida huwa ni kichefuchefu, kutapika na kuharisha. Baadhi hupatwa na homa ya baridi (inayoleta mzizimo).
NI MDA GANI UMUONE DAKTARI AU KWENDA HOSPITALI?
Kama kutatokea damu kuvuja kwa wingi sana (hali hii hutokea mara chache sana, kama asilimia 1, yaani chini ya mwanamke 1 kwa watu mia)

Kuvuja damu kwa wingi ni kule kunakoendelea kwa zaidi ya saa 2 hadi 3 na kuloanisha zaidi ya pedi 2 kwa saa (au kama damu inatiririka mfano wa maji ya bomba iliyo wazi).
Dalili za kupoteza damu nyingi mno ni pamoja na kizunguzungu au kusikia kichwa chepesi, na hali hii ni hatari kwa afya ya mwanamke.
Kama kunamaumivu yasiyokwisha siku chache baada ya kumeza dawa au kuvuja kusiko kwa kawaida ukeni

Dalili kama vile maumivu makali yanayoendelea kwa siku kadhaa na/au majimaji ya ukeni yenye harufu mbaya na/au kupatwa na homa huashiria mimba ambayo haikutoka vizuri. Hali hii hutokea pindi mimba imetoka lakini kukawa mabaki ya ujauzito tumboni na hii huitaji matibabu rasmi,
Mwanamke anaweza kuweka vidonge 2 au zaidi vya Misoprostol chini ya ulimi (asivimeze, aviache tu viyeyuke kwa dakika 30). Kama dalili zitaendelea baada ya kutumia vidonge hivi, mwanamke anapashwa kwenda mara moja kumuona daktari.
Kama mtu anavuja majimaji yenye harufu mbaya ni kawaida kwake kumuona daktari ili kupata matibabu ya dawa aina ya “antibaiyotiki”.
Kama umepatwa na homa

Homa ya baridi au mzizimo ni dalili ya kawaida utumiapo Misoprostol, ikiwemo pia joto kupanda. Ila iwapo mtu atapata homa ya zaidi ya nyuzijoto 38°C kwa kipindi kinachozidi saa 24, au kama atakuwa na homa ya zaidi ya nyuzitojo 39°C, ni lazima amuone daktari. Yawezekanaakawa amepatwa na maambukizi kutokana na utoaji mimba mabayo yanahitaji matibabu (kwa kutumia dawa za antibiotics na/au kuoshwa kizazi). Dawa inayotumiwa zaidi ni Doxycyline.

Iwapo yeyote atahisi kuna matatizo ni lazima aende kituo cha afya kilicho jirani au kuomba msaada wa daktari. Katika nchi ambako ni kosa la jinai kutoa mimba, haitamlazimu mwanamke kumweleza daktari kuwa alijaribu kutoa mimba. Mwanamke anaweza kumweleza kuwa mimba iliporomoka yenyewe. Daktari HATAWEZA kugundua tofauti. Tiba pia ni ileile. Mwanamke atasafishwa kizazi kwa kukoropwa na daktari. Ni jukumu la daktari kutoa huduma kwa kila hali inayokitokeza.
UFANYE NINI IWAPO MISOPROSTOL IMESHINDWA?

Kama Misoprostol imeshindwa kusababisha damu kuvuja au damu ilivuja kidogo tu huku mimba ikiendelea, mwanamke anaweza kurudia utaratibu mara nyingine (kama bado mimba yake iko chini ya wiki 12) na inawezekana akafaulu safari ya pili.
Kama mimba itaendelea baada ya jaribio la kutoa mimba kwa dawa hizi kuna uwezekano wa mtoto kuzaliwa na ulemavu wa mkono au mguu au matatizo ya mishipa ya fahamu.
NINI KITAFUATA?

Usiingize kitu chochote ukeni ndani ya siku 5 baada ya kutoa mimba (usifanye pia tendo la ngono) kwa kuwa inaweza kusababisha maambukizi. Baadaye unaweza kupata ujauzito mwingine. Lazima utumie majira ili kuzuia kupata mimba
nyingine usiyotarajia. Unaweza kutumia kondomu mara moja.
Unaweza pia kuomba daktari akuwekee vijiti vya majira (IUD) ukeni mara tu damu zinapokauka na kipimo cha mimba kuonyesha hamna ujauzito. Unaweza pia kumeza vidonge vya majira siku ileile utakayo tumia Misoprostol, lakini havitakuwa salama sana katika mwezi wa kwanza. Tumia pia njia zingine za majira kama vile kondomu kwa kinga zaidi ndani ya mwezi ule wa kwanza.

10 comments:

Alice said...

hallo
asante kwa ahabari hii, je naomba kujua kama vidonge hivi vinapatikana hapa bongo dar es salaam

asante

Anonymous said...

kwa kweli nimeappriciate maelezo yako kwasababu mimi mwenyewe ni mtumiaji mzuri na unachoeleza nisahihi.
Ila mbona hujawafundisha watu njia ya kuinsert vidonge hivi?Yakumeza ni ngumu sana.
Wewe ndo mkombozi. nashangaa watu wanoficha mbinu hizi wakati wanawake wanaangamia. Cshawishi watu watoe mimba bt kama bahati mbaya na mazingira yanabana kuliko kufa bora asaidiwe apte nafasi ya kujipanga sawasawa

Anonymous said...

jamani mie nataka kujua tu kama hivi vidonge vinapatikana wapi hapa tanzania!!

Anonymous said...

JAMANI NAOMBA MNISAIDIE NA MIMI NATAKA NITOE MIMBA MANA IMEINGIA WKT CJAJIPANGA BADO LKN NINA PRESHA JE NI SAWA KUMEZA HIVYO VIDONGE JAMANI NAOMBA MNISAIDIE WAPENZI

Anonymous said...

Dawa kwa hapa Dar es salaam kuna duka lipo mwenge shuka ITV halafu ulizia nakiete famasi, ila hawauzi hadi uandikiwe na daktari, sasa mashosti kama mnavyojua nirahisi wewe nenda dispensary mweleze hata daktari wa pale kama hauna dokta maalum akuandikie uende kununua bei ninafuu mno ila ukitaka kutumina nunua na antibiotics ili uanze pamoja mimi nazungumzia zile za kuinsert aina ya antibiotis nitawwaandikia kesho .Ila habari ndo hiyo kwa wanawake wenye hali ngumu kabisa ya mazingira ya kujifungua au ningumu kwao kulea mimba.
Please itumike pale tu inapobidi hii hata mwenyezi Mungu nae anaona usifanye kama mchezo wakununua nyanya sokoni..
POLENI WANAWAKE WENZANGU.

Anonymous said...

Dawa kwa hapa Dar es salaam kuna duka lipo mwenge shuka ITV halafu ulizia nakiete famasi, ila hawauzi hadi uandikiwe na daktari, sasa mashosti kama mnavyojua nirahisi wewe nenda dispensary mweleze hata daktari wa pale kama hauna dokta maalum akuandikie uende kununua bei ninafuu mno ila ukitaka kutumina nunua na antibiotics ili uanze pamoja mimi nazungumzia zile za kuinsert aina ya antibiotis nitawwaandikia kesho .Ila habari ndo hiyo kwa wanawake wenye hali ngumu kabisa ya mazingira ya kujifungua au ningumu kwao kulea mimba.
Please itumike pale tu inapobidi hii hata mwenyezi Mungu nae anaona usifanye kama mchezo wakununua nyanya sokoni..
POLENI WANAWAKE WENZANGU.

Anonymous said...

asante sana mamii kwa info hizo ila unajua ningejua gharama zake ningefurahi zaidi kwani siwezi kwenda kuuliza price ghafla tafadhali nisaidie hilo!!

maana kama usemavyo sio kwa matumizi ya ovyo bali ni pale inapobidi kwani wanawake wengi ktk ndoa wanateseka mno utakuta mtu ana mtoto mdogo kama miezi mi4 then anakamata tena na ujuavyo uzazi wa mpango wanaume wengi wanasema eti unapoteza hamu yaani utamu yaani ni balaa!!

asante kwa taarifa

Anonymous said...

jamani yule dada tunaomba atuelezee namna ya kutumia njia ya ku-insert vidonge vya kutoa mimba

Tanaagae said...
This comment has been removed by the author.
Anonymous said...

hivi jaman kama m2 unahisi una mimba kuna dawa ya kunywa ndan ya cku hiyo au kesho yake ili ic endelee